Thursday, September 18, 2014

MTABIRI ALITABIRIA PENZI LA RAY, CHUCHU

Na Gladness Mallya
MTABIRI maarufu nchini, Hassan Yahya Hussein amelitabiria penzi la waigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans kuwa litakuwa na mafanikio makubwa kwani wanaendana.
Waigizaji wa filamu Bongo Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans wakipozi.
Akizungumza na Amani, Hussein alisema kinyota Ray nyota yake ni aina ya Mashuke ambapo Chuchu nyota yake ni Mapacha ambazo zinaendana kwani wanashirikiana sayari moja ambayo ni Mercury na siku yao ya bahati ni Jumatano.
Mtabiri maarufu nchini, Hassan Yahya Hussein akiwa ndani ya ofisi za2dayhabari
“Japokuwa Ray amehangaika sana lakini kwa Chuchu amefika hivyo ajitahidi kutulia na asihangaike tena na wanawake kwani huyu wanaendana tofauti na wale wanaotajwa kuwa alikuwa na uhusiano nao yaani  Johari na Mainda,” alisema Hussein.

0 comments: