MSIKITI WA HINDU DAR WATEKETEA KWA MOTO
MSIKITI wa madhehebu ya
Wahindu uliopo maeneo ya Mtaa wa Kibasila karibu na shule ya Olimpia
jijini Dar es Salaam, umeteketea kwa moto leo asubuhi ambapo baadhi ya
mali zimeungua na mtu mmoja kukimbizwa hospitali kutokana na mshituko.
Akizungumza na mtandao huu, shuhuda mmoja
alisema moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye
mashine ya luku ambapo baadhi ya waumini walikuwa wakijiandaa kuupamba
msikiti huo.
0 comments: