Kufuru:Bunge Lakodi Vipaza Sauti kwa Sh8.9 Milioni Kila Siku
Wakati
kukiwa na malalamiko kwamba Bunge la Maalumu la Katiba linagharimu fedha
nyingi za walipakodi, uongozi wa taasisi hiyo umetumia Sh142.56 milioni
kukodi vipaza sauti kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha
(AICC).
Katibu
wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alithibitisha kukodiwa kwa vipaza
sauti hivyo kwa ajili kamati zote 12 na kwamba kila gharama ya chumba
kimoja kwa siku ni Dola 450 za Marekani (Dola moja ni wastani wa
Sh1,650).
Kwa
maana hiyo Bunge, hilo linatumia Dola 5,400 sawa na Sh8.91 milioni kwa
siku kugharimia vipaza sauti katika vyumba 12 vinavyotumiwa na kamati
hizo na kwa siku 16 ambazo kamati zitakutana, gharama hizo zitafikia
Sh142.56.
“Vifaa
vya sauti tulivyokuwa navyo vinalalamikiwa, vilikuwa siyo standard
(viwango) hasa vya mazungumzo, tumekodi kutoka Ukumbi wa Mikutano wa
AICC na tumekuwa nao usiku mzima kuvifunga,” alisema.
Alisema
tangu wavifunge, hawajawahi kupata malalamiko tena kutoka katika kamati
kuhusu ubora na kwamba gharama za kukodisha vifaa hivyo itatoka katika
fungu la dharura la Bunge Maalumu.
“Mara
ya kwanza walituambia gharama zao ni Dola 500 kwa siku lakini
tukajadiliana nao, hivyo tukafikia kiwango hicho cha Dola 450,” alisema.
Hamad
alisema vifaa vya awali ambavyo vililalamikiwa na wajumbe kuwa
havitoshi, vinatoa sauti nje ya majengo na kwa jinsi vilivyo,
vinalazimika kutembezwa ukumbini, hivyo kusababisha usumbufu.
Malalamiko ya gharama
Suala
la gharama limekuwa likiibuka mara kwa mara na wakati mwingine kutajwa
kama sababu ya kuahirishwa kwa Bunge hilo kwa kuwa hakuna uhakika wa
kupatikana kwa akidi inayotakiwa kufikia uamuzi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania
(Jukata), Deus Kibamba alilalamikia kile alichokiita “matumizi ya
kufuru” ya Bunge Maalumu wakati hakuna uhakika wa kupatikana kwa Katiba
Mpya.
0 comments: