Sunday, September 14, 2014

Nisiku nyingine tena tunakutana katika safu hii nikiamini umzima na unaendelea vizuri na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.Mimi namshukuru Mungu kwa kila jambo, amenijaalia afya njema na nguvu za kutosha kiasi cha kuweza kukuandikia wewe kile ambacho naamini kina umuhimu katika maisha yako ya kimapenzi. Leo ningependa tuzungumzie mambo ya kuzingatia kabla ya kumrudia mpenzi ambaye aidha mmeachana, yupo mbali na wewe au umepoteana naye kwa muda mrefu. Kugombana ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Yawezekana ulikuwa na mwenzi wako ambaye ulimpenda kwa moyo wako wote na sasa mmeachana lakini moyo wako bado unahitaji kuwa naye. Kutengana kuna mambo mengi, wakati mwingine huenda ilikuwa ni hasira tu. Siku zote baada ya hasira kuisha, moyo hubaki peke yake katika nafasi yake halisi ya kufanya maamuzi. Hapo ndipo penye lengo la mada yetu ya leo. Kwamba, kwa msingi huo umegundua kumbe mpenzi wako uliyeachana naye, bado unampenda. Kwamba hata makosa aliyokuwa akiyafanya, ulimsababishia au si makubwa kiasi cha kuachana na badala yake mnaweza kukaaa na kuzungumza kiutu uzima na kuyamaliza. Upo tayari rafiki? Je, uko katika kundi hilo? Unataka kumrudisha mpenzi wako wa zamani? Kama jibu ni ndiyo basi mada hii inakuhusu. HAKIKISHA BADO ANAKUPENDA Kwa utafiti mdogo nilioufanya nimebaini kuwa baadhi ya watu huamini kwamba kurudi kwa mara nyingine kwa mpenzi wa zamani ni kujidhalilisha, kujishusha na kujisalimisha. Hilo si kweli hata kidogo, kikubwa cha kuzingatia hapa ni moyo. Je, unahisi bado unampenda? Ni kweli naye anakupenda? Kama sifa hizi zipo, hayo mambo madogo ambayo mmetofautiana ni ya kawaida kabisa ambayo mnaweza kurekebishana taratibu. Kwa msingi huo basi, hakuna tatizo lolote katika kurudiana na mpenzi wako wa zamani, maana tayari mmeshajuana vya kutosha, hivyo kukupa urahisi wa kufanya yale anayoyapenda na kuepuka asiyopenda, jambo litakalozidisha umri wa uhusiano wenu. HAJAPATA MWINGINE? Lazima ujue kuhusu historia yake kiuhusiano baada ya kuachana na wewe. Hapo unatakiwa kufanya ushushushu wako kimyakimya bila yeye kujua. Ikiwa ameshatembea na mwingine, maana yake ni mtu asiye na msimamo na huenda anaongozwa zaidi na tamaa za kimwili na si mapenzi ya dhati. Katika kipengele hiki, ni muhimu sana kujua kama muda huo ambao wewe unahitaji kurudi tena mikononi mwake kama ana uhusiano mwingine. Kimsingi kama atakuwa ndani ya uhusiano, itakubidi uwe mpole. Unatakiwa kufanya hivyo kwa sababu anaweza kukubali kuwa na wewe wakati akiwa bado hajaachana na mpenzi aliyenaye kwa muda huo, hivyo wewe kuwa kama mwizi tu kwa mwenzako. Hapo utakuwa katika mapenzi ya kushea, jambo ambalo si zuri kisaikolojia na hata kiafya. Kumbuka kwamba, unaweza kuwa na mwenzi wako, mkapendana kwa dhati na mkadumu kwa muda mrefu, lakini kwa bahati mbaya mkaachana kwa sababu ambazo mnazifahamu wenyewe. Katika muda mfupi ambao utakuwa umeachana naye, anaweza kufanya mambo ya ajabu sana. Pamoja na kwamba moyo wako unamhitaji, lakini anaweza kuwa tayari ameshapoteza sifa za kuwa na wewe. Katika hali hiyo, ni sahihi kurudiana naye? Bila shaka jibu hapa ni siyo sahihi. ANA DHAMIRA YA NDOA? Huenda uliachana na mpenzi wako lakini bado unaamini ndiye alipangwa kuwa mwenza wako wa maisha, hiyo isiwe sababu, jiulize pia kama na yeye anahitaji kuingia kwenye maisha ya ndoa na wewe. Nasema hivyo kwa sababu, unaweza kunga’ang’ania kumrudisha mpenzi wako wa zamani kumbe mwenzako anataka kupitisha siku tu na wewe. Hana mpango wa kuishi na wewe kindoa. Kama utabaini mliachana lakini wote dhamira yenu ni kuoana, basi mrudie lakini kama unahisi ni mtu wa kustarehe tu na wewe na wala si muolewaji/muoaji, sidhani kama itakuwa sawa kumrudia. HANA KINYONGO? Wapo ambao wanafikia hatua ya kuachana baada kukoseana tena wakati mwingine makosa makubwa. Kwa maana hiyo kama wewe ndiye uliyemkosea mpenzi wako kabla ya kuanza jitihada za kumrudia, kwanza chunguza kama hana kinyongo na wewe na amekusamehe kutoka moyoni mwake? Kama bado ana kinyongo na ukalazimisha kurudiana naye, huwezi kulifurahia penzi lenu, itakuwa kila akikumbuka ulivyomkosea anapata maumivu na hawezi kukupenda kwa kiwango kinachotakiwa. Hayo ni baadhi ya mambo ambayo unatakiwa kuyazingatia kabla ya kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Cha kuzingatia sana ni kwamba rudiana na mtu ambaye una imani hamtakorofishana tena na kwamba kuachana kwenu kwa mwanzo kuwe kumewapa fundisho. Ni hayo tu marafiki, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine.

Kugombana ni jambo ambalo halikwepeki katika uhusiano wa kimapenzi. Upo ugomvi ambao ni wa kawaida na huisha kirahisi lakini upo ugomvi ambao huwa mkubwa na kama ukitokea na ukashindwa kujua nini cha kufanya kuweka mambo sawa, husababisha ufa kwenye penzi lenu.Leo tutazungumzia mambo muhimu ya kufanya inapotokea wewe na mpenzi wako mmeingia katika ugomvi mkubwa, mmetoleana maneno machafu au hata kupigana.
1. TAFAKARI CHANZO CHA TATIZO
Kuna usemi kwamba ukitaka kulitatua vizuri tatizo ni lazima kwanza ujue chanzo cha tatizo lenyewe. Ukishindwa kugundua chanzo cha tatizo, basi na wewe unakuwa sehemu ya tatizo.
Utashangaa kwamba wapenzi wengi hugombana na mambo kuwa makubwa kabisa kwa sababu ya vyanzo vidogo ambavyo walishindwa kuvigundua mapema na matokeo yake vikazaa matatizo mengine.
Mfano rahisi, chanzo kinaweza kuwa mpenzi wako amekupigia simu lakini ukashindwa kuipokea kwa muda muafaka. Atakapopiga kwa mara nyingine au mkikutana, usitegemee atakufurahia kwa sababu atahisi umemdharau kwa kutopokea simu yake.Endapo ukifanya makosa ya kushindwa kuliona kosa lako mapema na kushindwa kuomba radhi au kutoa maelezo yanayoeleweka kwa nini hukupokea simu, matokeo yake utamjibu vibaya, naye atakujibu vibaya na mwisho mtaishia kupigana au kuachana kabisa mkiwa mmeshatoka kabisa kwenye kosa la msingi.
Bila shaka msomaji wangu umeona jinsi chanzo kidogo kinavyoweza kusababisha tatizo kuwa kubwa. Ndoa nyingi au uhusiano unaofika mwisho huwa umesababishwa na mambo madogo ambayo yalishindwa kutafutiwa suluhu mapema.
Katika kila ugomvi unaotokea, jambo la kwanza jipe muda wa kutafakari chanzo kilichosababisha mkagombana. Wakati mwingine wewe ndiyo unaweza kuwa chanzo cha tatizo lakini kama ukiyajua makosa yako mapema na kukiri kisha kuomba radhi kwa mwenzio, utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kurudisha mapenzi kwa haraka.
2. MPE MUDA HASIRA ZIISHE
Kila binadamu ameumbwa akiwa na hasira na kwa bahati mbaya ni wachache wanaoweza kuzidhibiti hasira zao. Ni rahisi mtu kutukana, kupiga au kuharibu vitu akiwa na hasira.Baada ya kugombana, kila mmoja lazima atakuwa na hasira na njia pekee inayoweza kuepusha matatizo zaidi, ni kujipa muda na kumpa muda mwenzako ili hasira zipungue.
Kama mpo sebuleni na umetokea ugomvi, ni busara kwenda chumbani au nje mpaka hasira zako zikiisha. Ni makosa kulazimisha suluhu wakati kila mmoja akiwa na jazba kwani mtaishia pabaya zaidi.
Ukishaona hasira zako zimetulia na mwenzako naye ametulia, unaweza kuanzisha mada juu ya kilichosababisha mkagombana. Tumia lugha ya upole kwani endapo utakuwa ukifoka au kuzungumza kwa sauti ya juu, matokeo yake mtarudia tena kugombana.
3. MPE NAFASI YA KUZUNGUMZA
Huwezi kumuelewa mtu kabla hujampa nafasi ya kuzungumza na kumaliza kile alichokusudia kukisema. Endapo tatizo limetokea na upo kwenye hatua za kusaka suluhu, mpe mwenzako nafasi ya kueleza dukuduku lililopo ndani ya moyo wake.
Usimkatishe wala kumbishia chochote, muache aongee ulichomuudhi mpaka dukuduku lake liishe kisha na wewe jieleze kwa upole na sauti tulivu.
4. OMBA MSAMAHA
Hakuna silaha nzuri inayoweza kukusaidia kuushinda ugomvi wowote na kutuliza mambo kabla hayajawa mabaya kama kuomba msamaha. Neno ‘samahani’ ni dogo lakini lina maana kubwa kwa yule mtu anayelitoa na anayelipokea.
Hata kama unaona dhahiri kwamba kosa siyo lako, omba msamaha kwanza kisha baada ya hapo anza kumuelewesha mpenzi wako kwa upole. Lazima mwisho na yeye atayaona makosa yake na kukuomba msamaha, mtaweza kuepuka kuukuza ugomvi huo na kurudisha hisia za mapenzi.
5. USIWEKE KINYONGO
Endapo umeamua kuomba msamaha kwa mpenzi wako, au yeye amekuomba msamaha, samehe kwa dhati kutoka ndani ya moyo wako na sahau kile kilichotokea. Ni kosa kubwa kuweka kinyongo rohoni, yaani unamwambia kwamba umemsamehe wakati moyo wako bado una hasira naye. Ukisamehe kwa dhati, jifunze na kusahau kwani kusamehe kunaenda sambamba na kusahau.
Wazungu wanasema forgive and forget. Elewa kwamba mpenzi wako ni binadamu ambaye hajakamilika, wala si malaika.
Lazima atakuwa akikosea mara kwa mara, endapo utakuwa ukilimbikiza vinyongo, unafuga matatizo makubwa kwani siku nyingine akikukosea hata jambo dogo, utakumbushia na ya jana na juzi na mwisho ugomvi utakuwa mkubwa sana.
Kwa maoni, ushauri au swali nicheki kwa namba za hapo juu.
Endelea kulike: 
                        www.2dayhabari.blogspot.com

4 comments:

  1. Jina langu ni Lilian N. Hii ni siku ya furaha sana maishani mwangu, shukrani kwa msaada ambao Dk White alitoa, akinisaidia kupona mume wangu wa zamani na uchawi wake na uchawi wa mapenzi. Nilikuwa nimeolewa kwa miaka 6 na ilikuwa mbaya sana kwa sababu mume wangu alikuwa akinidanganya kweli na kutafuta talaka, lakini nilipopata barua pepe ya Dkt.White kwenye mtandao juu ya jinsi alivyosaidia watu wengi kupata tena ile ya kwanza na kusaidia kurekebisha uhusiano. na kuwafurahisha watu katika uhusiano wao. Nilimuelezea hali yangu na kisha kuomba msaada wake, lakini, kwa mshangao wangu, aliniambia kuwa atanisaidia katika kesi yangu na hapa nasherehekea sasa kwa sababu mume wangu amebadilika kabisa. Yeye siku zote anataka kuwa kando yangu na hawezi kufanya chochote bila zawadi yangu. Ninaipenda sana ndoa yangu, ni sherehe gani nzuri. Nitaendelea kushuhudia kwenye wavuti kwamba Dk White kweli ni mchezaji wa kweli wa spell. UNAHITAJI MSAADA KUOMBA SASA DAKTARI NYEUPE SASA Kupitia barua-pepe: wightmagicmaster@gmail.com. au WhatsApp Ndiye jibu pekee la shida yako na inakufanya ujisikie mwenye furaha katika uhusiano wako.
    1 UPENDO WA KWELI
    2 USHINDE ZARI NYUMA
    3 MATUNDA YA ASALI
    4 Spell ya kukuza
    5 USALAMA WA KUJIKINGA
    6 BIASHARA YA BIASHARA
    7 KAZI nzuri ya kazi
    8 Spell ya Bahati Nasibu na KESI YA KAMATI YA MAHAKAMA.
    wightmagicmaster@gmail.com

    ReplyDelete
  2. Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe nikiwa nimesimama peke yangu bila mwili kusimama na mimi na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na mchawi huyu wa hodari Dk. ASUBUHI, baada ya kumueleza hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi akiniomba kuwa hatawahi. niache tena, miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa pia una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
    *penda uchawi
    * kama unataka ex wako nyuma
    * Acha talaka
    *kuvunja mawazo
    * huponya viharusi na magonjwa yote
    * uchawi wa ulinzi
    *Ugumba na matatizo ya ujauzito
    Wasiliana na Dk DAWN kwa barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
    Whatsapp: +2349046229159

    ReplyDelete
  3. Kwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
    Anasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
    *Kama unataka kupata mimba.
    *Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
    *Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
    *Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
    *Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
    *Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
    Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159

    ReplyDelete
  4. Nilikuwa na uzoefu mgumu na wa kutisha katika mahusiano yangu ya awali na nilisubiri sana hadi nilipokutana na mume wangu na baada ya kukutana, tulipendana na kuoana. Baada ya miaka miwili ya muungano, alibadilika na kuanza tabia za ajabu na hatimaye kuniacha mimi na mtoto wetu. Nilifanya kila niwezalo kumrudisha lakini yote yalikuwa bure. Nilipata maoni mengi na kila mtu alikuwa akisema juu ya Dk Dawn. Niliwasiliana naye na alinijibu na kunipa juhudi zake zote na msaada ili kuifanya ndoa yangu ifanye kazi tena. Yeye ndiye aliyenijulisha kuwa mume wangu alichukuliwa kutoka kwangu na mwanamke mwingine na akafanya uchawi wa kuungana tena ambao uliturudisha pamoja na kurudi nyumbani kwangu na kijana wangu. Hakika, hakuna mtu huko alidanganya kuhusu Dk Dawn na matendo yake mema. Mume wangu alirudi nyumbani saa 73 baada ya kufanya kazi kama alivyoahidi. Wasiliana naye sasa na uwe na uhakika kwamba atakusaidia kuunganisha tena ndoa/uhusiano wako.
    Atakusaidia kushinda kesi mahakamani au kulipiza kisasi dhidi ya adui zako.
    Atakusaidia kuponya ugumba na kila aina ya magonjwa/magonjwa.
    Ana suluhisho la shida yako.
    Wasiliana na Whatsapp yake: +2349046229159
    Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete