Johari: Upofu wa kwenye Filamu ulinitesa
Alianza kuigiza tangu enzi za kundi la sanaa za maigizo la Kaole, lakini hajawahi kushuka kiwango katika uigizaji.
Huyo ni Blandina Chagula maarufu Johari, ambaye
mbali ya kuigiza amejaliwa kipaji akimudu vyema kuuvaa uhusika katika
uigizaji na kuonyesha tofauti kati ya huzuni na furaha.
Katika mahojiano yake na Starehe, Johari anaeleza
mambo mbalimbali asiyoweza kuyasahau katika uigizaji wake ikiwamo
kulibadili soko la filamu kutoka enzi za kutazamwa bure kupitia runinga
na sasa kuuzwa kwa wananchi.
Mkali huyo wa filamu anasema kuwa hataisahau tamthilia ya Johari, iliyobeba umaarufu na kumpa jina la usanii ‘Johari’.
Anasema anaikumbuka tamthilia hiyo kwa kuwa ndiyo
iliyowapa wazo la kubadili mfumo wao wa utendaji kazi kutoka tamthilia
walizokuwa wakiigiza na kuonyeshwa bure kwenye runinga na kuigeuza kuwa
biashara, ambapo badala ya shabiki kuvizia vipindi vya televisheni ili
aitazame vipande vipande, ataipata yote kwa kulipia akinunua Dvd.
“Ilikuwa ngumu sana, lakini kwa kuwa tulikuwa watu
makini akiwamo marehemu Steven Kanumba, msimamo ulikuwa huo. Kwa shida
mfumo huo ukakubalika na unafanya kazi vizuri hadi sasa na kuwapatia
mafanikio wasanii wa filamu kwa kiasi fulani, “anasema.
Johari anaitaja filamu iliyompa shida wakati wa
kuitayarisha kuwa ni ‘Yellow Banana’, ambapo aliigiza kama mlemavu
asiyeona (kipofu), huku ukweli akiwa anaona.
Anasema kuwa wakati wa kupiga picha za filamu hiyo
alipata wakati mgumu kwa kuwa kuna eneo, Vicent Kigosi (Ray),
aliyeigiza kama mumewe alimpiga kibao huku akitakiwa kutoonyesha kama
alikuwa anauona mkono uliokuwa ukija kumpiga, wakati ukweli ni kwamba
aliuona.
Johari anafafanua kuwa jambo jingine
analolikumbuka katika filamu hiyo ni pale alipoanguka kwenye ngazi, huku
Ray (mumewe), akiwa amekaa na kimada kwenye kochi.
Anaeleza kuwa kipande hicho kilikuwa kikimliza
hata akiwa peke yake kwani alianguka kweli hadi ngazi ya mwisho huku Ray
akimudu vyema kumtazama bila kushtuka kwa kuwa alilewa kwenye penzi la
kimada, baada ya yeye kuwa kipofu.
“Nilipata shida sana, kila anapotaka kunipiga
nakwepa, hivyo ilinichukua muda sana kufanikiwa kupata picha isiyokuwa
na chembe ya mshtuko. Lakini nilipoanguka kwenye ngazi na Ray kutulia
bila kushtuka. Roho iliniuma kama kweli, hata nilipokuwa nikilia,
nililia kwa hisia za kweli,” anasema Johari.
Anaeleza kuwa mbali na waigizaji kujituma kuna mambo yanayokatisha tamaa katika uigizaji.
www.2dayhabari.blogspot.com
www.2dayhabari.blogspot.com
0 comments: