Chaka Khan: Sauti iliyoacha historia kwenye miondoko ya Funk
Unapozungumzia muziki wa Funk, hutatenda haki kwa mashabiki ikiwa hutamtaja Chaka Khan ambaye ni miongoni mwa wasanii waliowahi kufanya vizuri kwenye miondoko hiyo.
Kutokana na umahiri katika muziki wake msanii huyo alijijengea umaarufu mkubwa katika miaka ya 1970.
Jina lake lilianza kuwika alipojiunga na Bendi ya Rufus, iliyokuwa na maskani yake mjini Chicago, Marekani.
Wengi tunamfahamu kama Chaka Khan au Malkia wa
Funk, lakini jina lake halisi ni Yvette Marie Sevens.Nyota huyu
alizaliwa Machi 23,1953.
Nyota huyu mzaliwa wa Chicago, alionyesha mapenzi
yake katika muziki tangu akiwa mdogo, jambo lililomfanya kufikiria
kuacha shule ili aingie kwenye fani hiyo iliyomfanya kuwa miongoni mwa
watu maarufu duniani.
Babu yake aliyekuwa akipiga muziki wa Jazz, ndiye
alichangia kwa kiasi kikubwa Khan kuingia kwenye muziki,akiwa na umri wa
miaka 11 tayari alishaanza kuonyesha kuvutiwa zaidi na miondoko ya
R&B na Blues.
Mwaka 1969, Khan aliacha shule na kuanza
kutumbuiza kwenye vikundi vya mtaani akiwa sanjari na mpenzi wake Hassan
Khan, ambaye baadaye walifunga ndoa.
Khan aliingia rasmi kwenye muziki mwanzoni mwa
miaka ya 70 akiwa mwanzilishi wa Kundi la Muziki la Crystalettes,
lililokuwa likiundwa na wasichana ndugu wa familia moja.
Hata hivyo, kundi hilo halikudumu sana kabla ya
kuvunjika na Khan kuhamia kwenye Bendi ya Rufus iliyokuwa ikisifika
wakati huo katika miondoko ya Funk.
Sauti nzito aliyokuwa nayo mwanamama huyu ilimpa
fursa ya kuwa muimbaji kiongozi katika bendi hiyo katika kipindi kifupi
alichojiunga nayo.
Huo ndiyo ukawa mwanzo wa Chaka Khan kuingia
kwenye ramani ya muziki wa Funk, hasa baada ya kuonyesha uwezo wa hali
ya juu katika kuitumia sauti yake tamu kuwachezesha mashabiki wa
miondoko hiyo.
Kupitia nyimbo ‘Tell Me Something’, ’Feel Good’,
‘Sweet Thing’, ‘Do you Love what you feel’ na nyinginezo Chaka Khan
alifanikiwa kuifanya Bendi ya Rufus kujizolea umaarufu mkubwa nchini
Marekani.
www.2tayhabari.blogspot.com
www.2tayhabari.blogspot.com
0 comments: