YANGA VS AZAM, MTOTO HATUMWI SOKONI LEO
PAZIA la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara linafunguliwa leo kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kwa Young Africans kucheza na timu ya Azam FC kwenye dimba la Uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Young Africans ambayo imekuwa na rekodi ya kufanya vizuri katika michezo ya Ngao ya Jamii, itashuka dimbani kupambana na wana lambalamba Azam FC huku ikiwa na kumbumbuku ya ushindi katika mchezo wa Ngao ya Jamii msimu…
PAZIA la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara linafunguliwa leo kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kwa Young Africans kucheza na timu ya Azam FC kwenye dimba la Uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Young Africans ambayo imekuwa na rekodi ya kufanya vizuri katika michezo ya Ngao ya Jamii, itashuka dimbani kupambana na wana lambalamba Azam FC huku ikiwa na kumbumbuku ya ushindi katika mchezo wa Ngao ya Jamii msimu uliopita ambapo watoto wa Jangwani waliibuka na ushindi wa bao 1-0, mtikisa nyavu akiwa ni Salum Telela "Essien".
Kikosi cha Azam FC.
Kocha Marcio Maximo ambaye atakuwa akiongoza Yanga mara ya pili
katika dimba la Uwanja wa Taifa amesema vijana wake wote wapo katika
hali nzuri jambo ambalo linampa wigo mpana wa kikosi kuchagua nani
amtumie katika mchezo wa leo.Naye Kocha Mkuu wa Azam FC, Joseph Marius Omog ameutaja mchezo wa leo kuwa ni mchezo muhimu. Omog amesema ni muhimu kwa timu yake kushinda mchezo wa leo ili kuimarisha morali ya timu kabla ya kuanza kwa ligi.
Azam inacheza mchezo huu kwa mwaka wa tatu mfululizo ambapo miaka miwili ya nyuma ilikuwa inacheza kama makamu bingwa na mara zote ilipoteza dhidi ya mabingwa Simba na Yanga, leo inacheza kama bingwa kwa hiyo Azam ina nafasi kubwa kushinda kama historia itatenda haki lakini pia kutokana na maandalizi na usajili uliofanyika.
Raia huyo wa Cameroun alisema amewapa wachezaji wake kila kitu kitakachowawezesha kushinda mchezo huo, kwa hiyo kazi imebaki kwao kushinda na kuleta furaha klabuni.
KIKOSI CHA AZAM LEO:
1. MWADINI ALI
2. SHOMARI KAPOMBE
3. ERASTO NYONI
4. DAVID MWANTIKA
5. AGGREY MORIS
6. BOLOU MICHAEL
7. HIMIDI MAO
8. SALUM ABUBAKAR
9. DIDIER KAVUMBAGU
10. KIPRE TCHETCHE
11. LEONEL SAINT PREUX
WALIO BENCHI:
AISHI MANULA
MUDATHIR YAHYA
SAID MORAD
GADIEL MICHAEL
ISMAILA DIARA
MCHA KHAMISI
KEVIN FRIDAY
KIKOSI CHA YANGA SC
1. Deo Munish "Dida" - 30
2. Juma Abdul - 12
3. Oscar Joshua - 3
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23
5. Kelvin Yondani - 5
6. Mbuyu Twite - 6
7. Said Juma "Makapu" - 22
8. Haruna Niyonzima - 8
9. Geilson Santos "Jaja" - 9
10. Mrisho Ngasa - 17
11. Nizar Khalfani - 16
WALIO BENCHI:
1. Juma Kaseja - 13
2. Salum Telela - 2
3. Edward Charles - 28
4. Rajaba Zahir - 4
5. Omega Seme - 14
6. Said Dilunga - 26
7. Saimon Msuva - 27
8. Hamis Thabit - 18
9. Hussein Javu - 21
10. Hamis Kizza "Diego" 20
www.2dayhabari.blogspot.com
1. Juma Kaseja - 13
2. Salum Telela - 2
3. Edward Charles - 28
4. Rajaba Zahir - 4
5. Omega Seme - 14
6. Said Dilunga - 26
7. Saimon Msuva - 27
8. Hamis Thabit - 18
9. Hussein Javu - 21
10. Hamis Kizza "Diego" 20
www.2dayhabari.blogspot.com
0 comments: