Wema: Kipilipili Kichwani Kwangu Kinanifanya Ninunue Mawigi
WEMA Sepetu ‘Beatiful Onyinye’ au Madam nyota katika tasnia ya filamu Bongo ametoa siri yake kuwa ni mteja mzuri wa mawigi badala ya kufuga nywele kama vile warembo wengine kutokana na kuwa na nywele za kipilipili.
Staa huyo anasema kuwa amejaribu sana kuzihudumia nywele zale hizo lakini mara nyingi hukatika, hivyo akaamua kunyoa kipara.
“Mara nyingi nikitengeneza nywele ni wiki moja tu nazitoa, siwezi kukaa na nywele muda mrefu kichwani kwangu, nilikuwa napenda kusuka au kutengeneza nywele zangu za asili, lakini sina nywele nzuri zangu ni kipilipili ndio maana natumia sana mawigi,”anasema Wema.
Wema anasema kuwa aliamua kuwa mfuasi wa mawigi baada ya pale alipokuwa akisuka nywele zake kukatika katika na kutumia muda mwingi kuzitibia bila mafanikio na yeye kujigundua kuwa hana nywele ndefu za asili pamoja kama angeamua kutengeneza haikuwezekana.
www.2dayhabari.blogspot.com
0 comments: