Thursday, September 25, 2014

MWANAMKE ALIPA MILIONI 33 KUONGEZEWA TITI LA TATU


Jasmine Tridevil katika pozi.
MWANAMKE aliyejitambulisha kwa jina la Jasmine Tridevil (siyo jina lake halisi) mwenye umri wa miaka 21 amedai kufanyiwa upasuaji na kuongezwa titi la tatu kupitia mahojiano aliyoyafanya redioni.

Jasmine ambaye ni raia wa Tampa jijini Florida nchini Marekani anayejishughulisha na utoaji huduma ya massage, alilipa kiasi cha dola za Kimarekani 20,000 sawa na milioni 33.4 za Tanzania kufanyiwa upasuaji huo.
Mwanamama huyo katika mahojiano na Real Radio 104.1 alidai kuwa ameamua kufanya hivyo ili asiwe na mvuto kwa wanaume maana hataki kuwa na mpenzi huku akipenda kuwa staa katika TV japo
alipoulizwa sababu ya kwa nini hataki kuwa na mwenza hakutaja sababu.

Takribani madaktari 50 walikataa kumfanyia upasuaji huo wakiogopa kuvunja miiko ya fani yao hivyo kumchukua miaka miwili kumpata daktari aliyekuwa tayari kufanya hivyo.
Kwa sasa mama huyo anarekodi video itakayoonesha changamoto anazokutana nazo akiwa mwanamke mwenye matiti matatu.
Mtaalam aliyemfanyia upasuaji ambaye hakutaka kutajwa jina lake alichukua tishu katika tumbo la mama huyo ili kutengeneza titi la tatu.
Jasmine amesambaza picha zake mpya akiwa katika vazi la bikini kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya upasuaji huo.
Mrembo huyo amedai kuwa amekanwa na mama yake mzazi pamoja na dada yake.
"Mama yangu alikimbia, hataki kuongea na mimi wala hataki dada yangu aongee na mimi baada ya kuongeza titi la tatu," Alisema Tridevil
Mbali na furaha aliyonayo mrembo huyo, bado anadai titi lake la tatu halifanani na mengine. Tridevil analazimika pia kujitengenezea mavazi yake mwenyewe ambapo ananunua mavazi mawili ya kuogelea
kisha moja analikata ili kupata nguo itakayokaa kwenye titi lake la tatu.

0 comments: