Friday, September 26, 2014

Maximo,Phiri hofu tupu



SIMBA ilipata sare, Yanga ikala kichapo, matokeo hayo yalikuwa ni katika mechi za ufunguzi wa Ligi Kuu Bara wikiendi iliyopita, habari ni kuwa sasa makocha wa timu hizo wapo kwenye presha kubwa ya kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi za wikiendi hii kwenye ligi hiyo.
Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo.
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo, yupo kwenye presha kubwa kutoka kwa mashabiki wake ambapo ili kupata ushindi, amewapa wachezaji mazoezi ya nguvu na kubadili mifumo ambayo hasa ameonekana…
SIMBA ilipata sare, Yanga ikala kichapo, matokeo hayo yalikuwa ni katika mechi za ufunguzi wa Ligi Kuu Bara wikiendi iliyopita, habari ni kuwa sasa makocha wa timu hizo wapo kwenye presha kubwa ya kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi za wikiendi hii kwenye ligi hiyo.
Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo.
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo, yupo kwenye presha kubwa kutoka kwa mashabiki wake ambapo ili kupata ushindi, amewapa wachezaji mazoezi ya nguvu na kubadili mifumo ambayo hasa ameonekana kuutumia mfumo wa ‘total football’ ambapo hadi washambuliaji wanarudi kukaba.
Wakati Maximo akikuna kichwa, upande wa pili Patrick Phiri ambaye ni kocha wa Simba, amesema ushindi ndiyo jambo kubwa katika mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya Polisi Moro, huku akielezea jinsi ambavyo amepanga kumtumia Amri Kiemba baada ya kuumia kwa Paul Kiongera.
Yanga imefanya usajili wa bei kubwa ikiwemo kuwasajili Wabrazili wawili, ndivyo ilivyo kwa Simba ambayo moja ya usajili wake gumzo ni wa Emmanuel Okwi aliyetokea Yanga, inaelezwa kuwa viongozi na mashabiki wa klabu zote wanahitaji ushindi ili upepo utulie, kinyume na hapo hali inaweza kuwa mbaya kwa makocha hao.
Geilson Santana ‘Jaja’.

Yanga ya Maximo
Katika mazoezi ya jana, Maximo aliwagawa wachezaji wake katika timu mbili na walikuwa wakicheza kama hawajuani kwa jinsi ilivyokuwa ‘kazikazi’. Mshambuliaji Geilson Santana ‘Jaja’ alikuwa timu moja na Mrisho Ngassa ambapo walionekana kuelewana vizuri.
Kutokana na kasi ya mazoezi hayo, Jaja akawa anarudi nyuma kukaba, pindi timu yake ilipokuwa ikishambuliwa huku Ngassa akibaki na mabeki wa upinzani, hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa upande wa pili, ambapo Simon Msuva alilazimika kurudi nyuma kukaba huku akimuacha Jerry Tegete mbele.
Emmanuel Okwi.

Wachezaji hao wa Yanga ambao watakipiga na Tanzania Prisons keshokutwa Jumapili baada ya kufungwa 2-0 na Mtibwa Sugar, walionekana kuwa na morali ya juu katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola jijini Dar.
Maximo pia alionekana kuwatumia Msuva na Andrey Coutinho katika kushambulia wakitokea pembeni na kuwapa tabu mabeki waliokuwa wakiwakaba kutokana na kuwa na kasi kubwa.

Kocha Mkuu wa timu ya Simba SC, Patrick Phiri kutoka Zambia.
Simba ya Phiri
Kutokana na kuumia kwa Kiongera katika mechi iliyopita dhidi ya Coastal Union iliyoisha kwa mabao 2-2, Phiri amelazimika kubadili mbinu ili kuhakikisha anarejesha furaha ya mashabiki kwa ushindi baada ya timu yake kufanya makosa mengi katika mechi hiyo ya kwanza.
Straika Paul Kiongera amekuwa akisumbuliwa na majeraha tangu akiwa KCB anatarajiwa kuwa nje kwa muda mrefu, ambapo Phiri amesema anatarajia kumtumia Kiemba ambaye katika mechi iliyopita aliingia dakika ya 89.
Simba ina majeruhi wengi, wengine ni; Haruna Chanongo, Abdi Banda, Issa Rashidi ‘Baba Ubaya’, Miraji Adam na Ivo Mapunda.
“Nimefanya marekebisho kadhaa, nimeanza kumpa mbinu Elias Maguli na Kiemba, pia kuna njia nyingine za kuwatumia Okwi na (Amissi) Tambwe tumekuwa tukizifanyia mazoezi.
“Ninajaribu mbinu mbalimbali ili ushindi upatikane, tangu jana (juzi Jumatano) katika mazoezi ya asubuhi. Safu ya ushambuliaji itakuwa na marekebisho makubwa pamoja na ulinzi ambayo ilicheza na kuonyesha kutoelewana katika mechi ya kwanza,” alisema Phiri.
Waandishi: Wilbert Molandi, Goodluck Ngai na Said Ally

0 comments: