AMANDA AZUA BALAA MTAANI
Stori: Chande Abdallah
Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni alizua balaa la aina yake baada ya kukatiza mtaani akiwa amevaa kigauni kilichokaribia kuacha wazi makalio yake.
Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni alizua balaa la aina yake baada ya kukatiza mtaani akiwa amevaa kigauni kilichokaribia kuacha wazi makalio yake.
Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ akiwacharukia wanaume waliokuwa wanampigia miluzi huku wakimzodoa.
Tukio hilo lililowashangaza wengi lilijiri eneo la Mwenge Bamaga
jijini Dar wakati msanii huyo alipokuwa akitembea kuelekea kwenye
mgahawa uliopo eneo hilo.
Huku akitembea…

Huku akitembea kwa staili ya
‘hamsini…mia…hamsini…mia…’, Amanda alionekana kufanya makusudi kwani
kadiri wanaume walivyokuwa wakijikusanya kumshangaa, ndivyo alivyoongeza
mikogo na kuwaacha miudenda ikiwatoka.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanaume ambao wengi wao ni madereva
wa Bajaj na mafundi gereji walionekana kumzodoa huku wakieleza kuwa, ni
msanii asiyejiheshimu.
“Yule kutuvalia sisi vile ndiyo nini?
Mavazi yale yanavaliwa klabu usiku tena wanaovaa vile ni wale
wasioithamini miili yao, tukisema anatutangazia biashara tutakuwa
tunakosea?” alihoji fundi mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma.
Katika kujua sababu ya kuvaa kigauni hicho, mwandishi wetu alimfuata
Amanda lakini kabla ya kuulizwa chochote aliingia kwenye gari na
kuondoka zake baada ya kuwachimba mkwara waliokuwa wakimpigia miluzi.
Baadaye alipopigiwa, simu iliita bila kupokelewa.
0 comments: