Monday, October 6, 2014

Tofauti na Ilivyofikiriwa Diamond Aonyesha Live Hadharani Kuwa Anamkubali Shem Wake Petit Man

Stori: Mayasa Mariwata
HESHIMA! Tofauti na ilivyokuwa ikifikiriwa na wengi kwamba hamkubali shemeji yake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameonyesha kumkubali shemeji yake Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ hadharani.

Hivi karibuni uvumi uliibuka kuwa Diamond hakufurahishwa na kitendo cha dada’ke kuolewa na Petit ndipo msanii huyo alipoamua kukata ‘vilimilimi’ kwa kusema uvumi huo hauna ukweli katika sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika Oktoba 2, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Posta jijini Dar.

“Kwa bahati mbaya dada yangu Esma anaumwa hajafika humu ndani, sasa kwa kuwa sasa hivi ameolewa na mtu ninayemkubali, namuita mumewe, shemeji yangu ninayemkubali, Petit Man aje kula keki badala yake,” alisikika Diamond.

0 comments: