Monday, October 13, 2014

Mwigizaji Wastara Amuumbua Shija Kwa Kusema Uongo

Stori: Pleasure Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Wastara Juma amemuumbua msanii mwenzake Deogratius Shija baada ya kutoa taarifa zinazoonekana ni za uongo.

Awali Wastara ambaye hivi karibuni alinyakua tuzo ya Muigizaji Bora wa Kike wa mwaka kwenye tuzo za Action and Cuts, alimshukuru Mzee Majuto kwamba ndiye aliyemtoa kisanaa jambo ambalo limemhuzunisha Shija na kusema anashangaa kwa kuwa yeye ndiye aliyemtoa.

Kufuatia maelezo hayo, Wastara amesema, taarifa aliyoitoa Shija ni ya uongo kwani  filamu ya kwanza kabisa alicheza na Mzee Majuto ndiyo maana alimshukuru, ya pili alicheza na Frank Mwikongi na ya tatu ndiyo ya Shija.

Nimemshukuru Mzee Majuto kwa kuwa ndiye wa kwanza kunitoa, huyo Shija nimecheza naye filamu ya tatu, sasa anacholaumu nini? Mimi huwa sipendi lawama za kijinga,” alisema Wastara.

0 comments: