Friday, October 10, 2014

‘Mtanzania aliondoka Chelsea siku nyingi tu’




Mtanzania aliyekuwa akiichezea timu ya vijana ya Chelsea ya England, Adam Nditi.
Na John Joseph

HABARI ni kuwa Mtanzania aliyekuwa akiichezea timu ya vijana ya Chelsea ya England, Adam Nditi, alishaondoka Chelsea zaidi ya miezi minne iliyopita na siyo mwezi uliopita.
Nditi ambaye alizichezea timu za vijana za klabu hiyo ya London, ikiwemo ile ya chini ya umri wa miaka 21, aliondoka Chelsea tangu mwezi wa sita mwaka huu na tayari…

Mtanzania aliyekuwa akiichezea timu ya vijana ya Chelsea ya England, Adam Nditi.
Na John Joseph
HABARI ni kuwa Mtanzania aliyekuwa akiichezea timu ya vijana ya Chelsea ya England, Adam Nditi, alishaondoka Chelsea zaidi ya miezi minne iliyopita na siyo mwezi uliopita.
Nditi ambaye alizichezea timu za vijana za klabu hiyo ya London, ikiwemo ile ya chini ya umri wa miaka 21, aliondoka Chelsea tangu mwezi wa sita mwaka huu na tayari taarifa kutoka klabuni hapo ilitolewa kipindi hicho.
Hiyo inamaana kuwa, Nditi hakuondoka mwezi uliopita kama ilivyoripotiwa (siyo na Championi), huku kaka wa mchezaji huyo akiliambia gazeti hili kuwa, mara ya mwisho Nditi alikuwa nchini Italia kwa ajili ya kuangalia ramani nyingine ya maisha yake ya soka.
Ripoti ya Chelsea ambayo ilitolewa Juni, mwaka huu, inaonyesha kuwa Nditi aliondoka Juni baada ya benchi la ufundi kuamua kumweka kwenye orodha ya walioondolewa kikosini licha ya kuwemo kwenye orodha ya wachezaji walioisaidia Chelsea kutwaa Kombe la FA la vijana.
Kaka wa Nditi ambaye amejitambulisha kwa jina la Cartius Calos Mbiku, alizungumza na gazeti hili na kufunguka kama ifuatavyo: “Mara ya mwisho alikuwa Italia akitafuta timu, ngoja nikutumie namba yake sasa hivi, lakini Chelsea alishaondoka siku nyingi tu.”Championi Ijumaa lilipomtafuta Nditi, simu yake haikupatikana hewani.

0 comments: