WEMA, DIAMOND WANADAIWA KUMWAGANA!
Diamond..Mh! Upepo mbaya
unaivumia kapo ya mafahari wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambapo wanadaiwa kufanyiana ‘taimingi’
ya kumwagana.
Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu makini,
wawili hao wamepotezeana kwa muda mrefu huku kila mmoja akifanya yake
lakini kila mmoja anashindwa kujitoa mhanga na kusema hawapo pamoja
akihofia kuonekana ndiye tatizo.
“Kifupi ni kwamba Wema na Diamond
hawapo pamoja kwa kipindi kirefu, yawezekana wanawasiliana lakini si kwa
mapenzi labda kwa mambo mengine. Diamond anazuga kama yuko kwenye shoo,
hata akirudi Bongo hawana ukaribu na Wema kama ilivyokuwa zamani,
anazuga kidogo kisha anaondoka tena.
Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinum.
“Wema naye hivyohivyo, yupo bize na
mambo yake, inasemekana yupo na kigogo f’lani hivi Mkongomani ndiye
anampa jeuri mjini kama ulivyoona juzikati amemwaga mapesa ukumbini.
“Inasemekana Mkongomani huyo
amemfungulia pia ofisi mpya ya kurekodia filamu pamoja na kumnunulia
gari jipya,” kilidai chanzo hicho.
Chanzo hicho kilikwenda mbele zaidi kwa
kudai kwamba, Jumapili (jana) Wema alipanga kutangaza rasmi kumwagana
na Diamond wakati alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa sambamba
na kumtangaza mwanaume wake mpya.
“Jumapili (jana) ndiyo kila kitu
kitakuwa hadharani maana Wema amepanga kutangaza hadharani kwenye
bethidei yake,” kilizidi kudai chanzo hicho.
Diamond na Wema wakila ujana.
Mwanahabari wetu alipokutana na Wema
nyumbani kwake na kumuuliza kuhusu madai hayo aliyakanusha yote lakini
akawa mzito kidogo katika suala la kutoonana muda mrefu na Diamond.
“Madai yote hayo siyajui! Nina bwana
mpya? Eti kaninunulia gari! Amenifungulia ofisi! Sijui nimeachana na
Diamond! Hayana ukweli wowote,” alisema Wema kwa mshangao mkubwa.
0 comments: