WEMA ALIPOWAFANYIA SHOPING MBWA YA MIL 6
KWA wale wenye hali ngumu kimaisha wataishia kusema; ni kufuru iliyoje kwani staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu hivi karibuni amewafanyia mbwa wake wawili ‘shopping’ iliyogharimu dola 4,000 za Kimarekani (zaidi ya Sh. milioni 6.5 za madafu).
Wema aliteketeza kiasi hicho cha fedha kwa kuwanunulia mbwa hao pafyumu,
viatu na nguo, alivyoagiza kutoka nchini China, lengo likiwa ni
kuhakikisha wanaishi katika mazingira mazuri.
Akizungumzia ‘shopping’ hiyo nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar,
Wema alisema: “Kiukweli nawapenda sana hawa mbwa, ukinipasua roho yangu
utawakuta ndiyo maana nataka wavae na kunukia vizuri, kinyume chake
siwezi kuwa na amani.
“Najua watu wanaweza kushangazwa na kitendo cha mimi kutumia kiasi hicho
cha fedha lakini sioni kama ni tatizo kwani ni kitu ambacho kinanipa
furaha katika maisha yangu.”
0 comments: