Friday, September 19, 2014

USICHOKIJUA KUHUSU THEA



Makala: Gladness Mallya

Mpenzi msomaji wa safu hii ya Exclussive Interview baada ya kumaliza kusoma historia ya maisha ya msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma, leo tunakuletea msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.Thea amefunguka mengi kuhusiana na maisha yake ya sanaa, karibu uinjoi mahojiano:
Msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.
HISTORIA KWA UFUPI

Nimezaliwa mwaka 1982 mkoani Shinyanga, nimepata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi…
Makala: Gladness Mallya
Mpenzi msomaji wa safu hii ya Exclussive Interview baada ya kumaliza kusoma historia ya maisha ya msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma, leo tunakuletea msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.Thea amefunguka mengi kuhusiana na maisha yake ya sanaa, karibu uinjoi mahojiano:
Msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.
HISTORIA KWA UFUPI
Nimezaliwa mwaka 1982 mkoani Shinyanga, nimepata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Igunda iliyopo Kahama ambapo nilisoma mpaka darasa la tatu na baada ya hapo nilihamia Shule ya Msingi Mapambano-Sinza, jijini Dar na kufanikiwa kuhitimu darasa la saba.
SEKONDARI            
Baada ya kuhitimu nilijiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Zanaki ambako nilisoma kwa mwaka mmoja tu na kuhamia Sekondari ya Gorio ambako nako nilisoma kwa mwaka mmoja nikahamia Kijitonyama ambako nilimalizia kidato cha tatu na cha nne.
APATA UJAUZITO
Baada ya kuhitimu kidato cha nne niliendelea kusoma masomo ya Pre Form Five lakini ndoto zangu zilikwamia hapo baada ya kupata ujauzito.
BAHATI MBAYA
Ilitokea bahati mbaya tu na sikuona sababu ya kutoa mimba ndiyo nikaamua kuzaa na nikapata mtoto wa kiume ambaye kwa sasa baba yake alimchukua anasoma Dubai.
Mimba hiyo niliipata mwaka 2003 nikiwa najiandaa na masomo ya kuingia kidato cha tano, nilipata ujauzito na kuamua kuzaa ambapo nilipata mtoto wa kiume anayejulikana kwa jina la Maron Bimpela.
HAWAKUWA NA MALENGO YA NDOA
Sisi hatukuwa na malengo ya kuoana bali nilipopata ujauzito na kujifungua baba mtoto aliendelea kumtunza mtoto mpaka alipokuwa mkubwa akaja kumchukua, ndoto zangu za kusoma ziliishia hapo.
RASMI KWENYE SANAA
Baada ya kujifungua sikuendelea tena na masomo bali niliendelea na sanaa kwani tangu nikiwa kidato cha nne nilikuwa nafanya sanaa hivyo niliingia rasmi.
AKUTANA NA CHIKI
Kwa mara ya kwanza kabisa Chiki Mchoma ndiye aliyenichukua akanipeleka kwenye kundi lililokuwa linajulikana kwa jina la Tunda.
MCHEZO WAKE WA KWANZA
Mchezo wa kwanza kushiriki na kurushwa Runingani uliitwa Ulimwengu wa Vijana ukweli siku hiyo sikulala kutokana na furaha niliyokuwa nayo. Kwenye kundi hilo nilidumu kwa muda mfupi sana, kama miezi tu.
AJIUNGA NA MAMBO HAYO
Baada ya hapo nilijiunga na Kundi la Mambo Hayo baadaye Kaole na hapo mpaka sasa naendelea kucheza filamu ambapo nina filamu za kwangu mwenyewe sita na nyingine zaidi ya 40 za kushirikishwa.
UHUSIANO NA BABA MTOTO
Baada ya kujifungua sikuendelea na uhusiano na baba mtoto wangu. Uhusiano uliokuwepo ni kwamba alikuwa akimlea mwanaye tu na baada ya kukua ndipo akamchukua.
AACHANA NA WANAUME
Baada ya kupata mtoto wangu nilitulia na kumlea na sikuwahi kujihusisha kimapenzi na mwanaume yeyote.Nilikaa miaka mingi sana mpaka nilipokuja kukutana na Michael Sangu ‘Mike’, tukafunga ndoa.
WALIVYOKUTANA
Mimi na Mike tulikuwa kwenye kundi moja ambapo nilikuwa namuita kaka na yeye ananiita mdogo wake lakini alikuwaga ananitania kwamba lazima atanioa nikawa naitikia kiutani tu.
Yaani sikuwa hata na wazo la kuolewa na msanii na nilikuwa nimeshaapa kwamba sitaolewa na msanii sijui ni kitu gani kilitokea maana Mike nilikuwa nimemzoea namuita kaka tukawa tunapiga stori sana lakini kila wakati alikuwa akiniambia atanioa nikawa namjibu sawa.

Itaendelea wiki ijayo!

0 comments: