Ugonjwa wa Ebola Watua Marekani, Mgonjwa wa Kwanza Agundulika
Mgonjwa
 wa kwanza wa ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola amegundulika nchini 
Marekani, imethibitishwa katika mji wa Dallas, Texas.
Maafisa
 katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian 
wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo.
Mgonjwa
 huyo anasemekana kuwa ni mtu anayeaminika kuambukizwa ugonjwa huo 
nchini Liberia kabla ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo.
Zaidi 
ya watu 3,000 tayari wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola huko 
Afrika Magharibi na idadi ndogo ya wafanyakazi wa Marekani wa mashirika 
ya misaada wamepata nafuu baada ya kupelekwa kutibiwa Marekani.
Jumatatu,
 maafisa wa kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian ya
 Dallas wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa jina alikuwa akichunguzwa 
virusi vya Ebola na ametengwa katika hospitali hiyo.
Shirika
 la Afya Duniani, WHO limesema mpaka sasa zaidi ya watu 3,000 wamekufa 
kutokana na virusi vya Ebola, wengi wa waliokufa ni kutoka Liberia.
Nchini 
Nigeria, nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kuna wagonjwa 19 
waliothibitika kuugua ugonjwa wa Ebola na watu wanane wamekufa tangu 
mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa nchini humo mwezi Julai..
Kuna mgonjwa mmoja aliyethibitika nchini Senegal, lakini hakuna taarifa za kifo mpaka sasa.
Ebola ni ugonjwa hatari wa virusi kuwahi kuzuka duniani.
 
 
 
 
0 comments: