Monday, September 29, 2014

TBS: Wananchi Acheni Kununua Nguo za Mitumba

Shirika la Viwango (TBS) limewataka wananchi kutonunua nguo za ndani za mtumba ili kuua soko la bidhaa hizo zenye athari kiafya.

Kaimu mkurugenzi anayehusika na udhibiti ubora wa TBS, Mary Meela alisema nguo hizo ni hatari kwani zinaweza kueneza magonjwa mbalimbali hasa ya ngozi.

Alisema lengo la ombi hilo ni kukomesha uuzaji wa nguo hizo ambazo zinaweza kusababisha maambukizi kutoka kwa aliyekuwa anavaa nguo hiyo kwenda kwa mtu wa pili.

Meela alisema shirika lake linashindwa kukomesha biashara hiyo kwa sababu halijapewa nguvu za kisheria kukataza watu kufanya biashara hiyo kama ilivyo Zanzibar, hivyo amewataka wananchi kutambua madhara hayo na kuacha kununua.

“Nguo za ndani zina bei ndogo hata mtu wa chini anaweza kumudu. Sioni sababu ya mtu kwenda kununua za mtumba,”

0 comments: