SERIKALI ZA TANZANIA NA MALAWI ZASEMA HAZINA TOFAUTI JUU YA MPAKA WA ZIWA NYASA
Balozi
wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere Akizungumza na waandishi wa
Habari kutoka Mbeya walipotembelea Ofisi za ubalozi Nchini Malawi.
Baadhi ya Waandishi wakimsikiliza Balozi.…
Baadhi ya Waandishi wakimsikiliza Balozi.
Baadhi ya Waandishi wa Habari Kutoka Mkoani Mbeya wakimsikiliza Balozi kwa Makini.
Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akipokea Taarifa kutoka kwa waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya.
Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mh. Patrick Tsere akijibu Taarifa ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya.
Waziri
wa Habari , Utalii na Utamaduni Nchini Malawi Mh. Kondwani Nankumwa
akiongea na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya Ofisini kwake.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya wakifuatilia Hotuba ya Waziri
wa Habari, Utalii na Utamaduni Mh. Kondwani Nankumwa.
Wa kwanza Kulia ni Afisa Habari wa Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni akifuatilia Mkutano huo.
Waandishi wa Habari wakiendelea kufuatilia Kikao hicho.
Francis
Phiri wa kwanza Kulia ambaye ni Mratibu wa ziara hiyo Nchini Malawi na
Muasisi wa Nyika Press Club ya Malawi akiwa katika Mkutano huo.
Kikao kikiwa Kinaendelea.
Waziri
wa Habari, Utalii na Utamaduni Nchini Malawi Mh. Kondwani Nankumwa wa
pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi
wa Habari Kutoka Mkoa wa Mbeya nje ya Ofisi yake Jijini Lilongwe.
Waziri wa Habari,Utalii na Utamaduni nchini Malawi Mheshimiwa
Kondwani Nankhumwa alisema kuwa Serikali ya Malawi haina mgogoro na
Serikali ya Tanzania kuhusiana na mpaka wa ziwa Nyasa.
Aliyasema hayo baada ya kukutana na Jopo la Waandishi Habari wa
Mkoa wa Mbeya waliotembelea ofisini kwake katika mfululizo wa ziara ya
waandishi waliofanya ziara ya juma moja nchini humo katika ziara ya
kubadishana uzoefu baina ya Waandishi wa Nchi hizo.
Waziri Nankhumwa alisema kuwa Mtoto wa Rais wa Malawi Profesa
Ather Muthalikana anasoma Dar es Salaam naye Rais amekuwa Muhadhiri wa
chuo kikuu na kwamba Watanzania wengi wanaishi na kufanya biashara
nchini Malawi hivyo hakuna sababu za kuwepo kwa tofauti za aina yoyote
ile itayowapelekea kuwagawa wananchi wa pande hizo.
Aidha alisema kuwa ili kuonesha hakuna tofauti baina ya wananchi wa
pande hizo Marais wa nchi hizo watapaswa kuchukua ndoano na kuvua
samaki pamoja katika ziwa hilo ili kuionesha Dunia kuwa wananchi wa
pande hizo ni wamoja na kuna mwingiliano wa makabila.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Balozi wa Tanzania nchini Malawi
Patrick Tsere ambaye alisema kuwa hakuna mgogoro wa mpaka katika Ziwa
Nyasa baina ya Tanzania na Malawi.
Aliyasema hayo alipotembelewa na waandishi wa Habari wa Mkoa Mbeya
walipotembelea ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi katika mfulizo
wa ziara ya waandishi hao nchini Malawi ili kubadilishana mawazo na
changamoto mbalimbali zikiwemo za mazingira,utalii na Elimu juu ya
Ukimwi ambazo zinafanana katika nchi hizo.
Balozi Tsere alisema hivi sasa si wakati wa marumbano kwani
inahitajika subira katika mzungumzo yaliyonza baina ya viongozi wa nchi
hizo na kwamba si wakati wa kuupeleka mgogoro huo katika mahakama ya
kimataifa ambapo utazigharimu fedha nyingi nchi hizo katika utatuzi wa
mgogro huo.
Hata hivyo Waandi wa Habari wa nchi hizo walifanya makubaliano
ambayo yatasaidia kuzitangaza nchi hizo kimataifa ikiwa ni pamoja na
mbuga za wanyama zilizopo Malawi na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Songwe ili utumiwe na wananchi hizo ili kukuza uchumi wan chi hizo.
Katika ziara hiyo Waandishi wa vyombo mbalimbali walishiriki ikiwa
ni pamoja na Tone Multimedia Group, Mbeya yetu Blog,Chanel
Ten,Mwananchi,Jambo leo,Bomba Fm,Majira na Raia Mwema.
Vingine na Tanzania Daima,Baraka FM na Mwandishi Rais mstaafu
Ulimboka Mwakilili ambaye alikuwa Mwenyekiti wa safari na Mhandisi wa
Ujenzi Claudio Lusimbi ambaye ni Mlezi Katika Safari hiyo
Na Mbeya Yetu Blog , Lilongwe Malawi.
Kawaidawww.2dayhabari.blogspot.com
0 comments: