SCOTLAND YAKATAA KUJITENGA NA UINGEREZA
Wananchi
wa Scotland waliokuwa wakitaka kujitenga na Uingereza wakiangua kilio
huku walioshinda wakiwa na furaha baada ya matokeo kutangazwa.
MATOKEO ya kura za
maoni nchini Scotland yametoka, kura 1,914, 187 sawa na 55% wamepinga
kujienga na Uingereza huku kura 1,539,920 sawa na 45% wakitaka
kujitenga.Kwa matokeo hayo, Scotland itaendelea kuwa sehemu ya Uingereza na Waziri Kiongozi wa Scotland Alex Salmond amesema ameridhia kuanguka katika mchakato wa kura ya maoni.
0 comments: