MATEKA MWINGINE AKATWA SHINGO NA KUNDI LA KIISLAM
Serikali ya Uingereza imesema kuwa
inachukua hatua za dharura ili kubaini ukweli wa kanda ya video
inayoonyesha mateka wa Uingereza David Haines aliyetekwa nyara na kundi
la himaya ya kiislamu akikatwa kichwa.
Mfanyakazi huyo wa misaada aliyekamatwa nchini Syria mnamo mwezi Machi mwaka jana ameonyeshwa akipiga magoti katika jangwa, kando yake akiwa na mtu aliyeficha uso wake ambaye amebeba kisu.
Atakuwa mateka wa tatu wa magharibi kukatwa kichwa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
katika kanda hiyo ya Video mtu aliyeshika kisu anaonekana akishutumu mataifa yanayounga mkono Marekani,naye Haines ambaye anaonekana kuwa chini ya shinikizo anaonekana akimlaumu waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron kwa hatma yake.
Mwisho wa kanda hiyo mateka wa pili wa Uingereza anaonyeshwa na kutishiwa.
Wakati huohuo Waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron ameshutumu kukatwa kichwa kwa David Haines kama kitendo cha kishetani.
Amesema kuwa wauaji watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria hata iwapo itachukua mda mrefu.
Katika taarifa yake Rais Obama pia ameshutumu mauaji ya kikatili ya David Haines.
Amesema Marekani inaomboleza na Uingereza kifo cha mateka huyo na kuongezea kuwa itashirikiana na muungano mkubwa wa kimataifa ili kuwakamata washukiwa mbali na kuharibu tishio hilo kwa ulimwengu.
Wanahabari wawili Steven Sotlof na james Foley waliuawa na wapiganaji hao mwezi uliopita.
www.2dayhabari.blogspot.com

0 comments: