MAHUSIANO: WADADA SOMO LA BURE KWENU,SOMA HAPA
Jamani wee, kila nikitaka kukaa kimya mdomo unanicheza, siwezi kukaa kimya moja kwa moja lazima nitie neno ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa. Kufunga kwetu bado hakusimamishi mapenzi ndani ya nyumba zetu, hivyo siwezi kukaa kimya huku naona jahazi linazama.
Leo wari wangu nataka niwape somo la bure kuhusu kulinda nyumba zetu. Tunalalamika kuwa waume zetu hawaoneshi kufurahia mapenzi tukiwa faragha. Inawezekana uliyenaye ni mgeni wa mambo ya chumbani, nawe kama siyo mbunifu wa kujua uliyenaye ni ‘maimuna wa mapenzi’ basi penzi lenu linakuwa bora liende.
Waweza usione hasara zake mapema, lakini huwa kubwa, ndicho chanzo cha nyumba nyingi kuyumba au kusambaratika kabisa. Unajua sababu gani?
Nakuuliza acha kunitumbulia mijicho kama fundi saa aliyepoteza lensi. Siku zote wachawi wa uhusiano wetu huwa sisi wenyewe, bila kujua tunaziroga ndoa zetu au uhusiano wetu.
Hebu kaa chini nikupashe ili usichelewe kumpikia futari na uji, basi uongeze cha ziada ili upate zaidi ili panapo majaaliwa umeremete kwenye sikukuu ya idd au usiye muislamu uamshe furaha na kumfanya mwenzako achanganyikiwe na kuona mambo mapya ya kimahaba.
Si wote mmepitia unyagoni na kupata mafunzo ya chumbani, jamani mafunzo ya chumbani ukiyajua nina imani ndoa yako kila siku itakuwa mpya. Katika maisha ya ndoa hasa ya chumbani lazima mwakwetu ujue wanaume wanapenda nini? Na hii utaijua pale mwanaume wako wa kwanza utakayekula naye raha umuulize kijanja vitu gani anapenda siyo kukurupuka kama unatoka kujisaidia kichakani.
Siku zote mjenzi mzuri hujifunza tabia za udongo ili akijenga nyumba isianguke haraka au kuweka nyufa. Hata katika mapenzi ukiwa faragha na mwenzako hebu jenga tabia ya kudadisi.
”Mpenzi nikikushika wapi unajisikia raha?” lazima atakujibu vilevile nawe una haki ya kumueleza mpenzi wako kuwa:
“Mpenzi wangu usisumbuke sana kunipapasa mwili mzima mi sehemu zangu hizi, ukinigusa sehemu hizi kama umetwanga pilipili lazima nikohoe.”
Umeona siyo mtu anakushika sehemu nyingine wala hazina msisimko unamuacha pengine naye Maimuna hajui lolote alipokushika ndipo uwezo wake wa kujua sehemu za kumsisimua mwanamke.
Kwa vile hajui basi utajikuta mpaka mchezo unaanza mwili wako bariiiidii. Haipendezi hebu basi tuambiane ukweli ili kuifanya nyumba yetu kila mara iwe na furaha.
Kuna maeneo mengi ya mambo ya chumbani unatakiwa kuyajua mkiwa kitandani. Unapoona hutendewi haki mweleze mwenzako ili ajue siyo kukaa kimya unaumia moyoni kumbe ulitakiwa kusema.
Wengi hulalamika hawajawahi kufurahia tendo la ndoa tangu waolewe hata wengine kudiriki kusema huwa hawafiki mwisho wa safari, mmh! Kioja.
Narudia kauli yangu, siyo wote wanaojua mapenzi, hebu muulize mtu aliyekuzidi amewezaje kufurahia mapenzi muda wote. Akishakueleza basi lifanyie kazi ndani, haki ya nani utashangaa kumuona mtu mzima akilia kama mtoto mdogo, si kwa kupigwa bali kutu ya mapenzi imeondolewa sasa hivi chuma kimekuwa laiiiini raha kila kona.
Utashangaa unapata ambavyo hukuwahi kupewa, la muhimu ni kukubali kujifunza na kuyafanyia kazi, hakika kila siku ndoa yako itakuwa mpya.
Yangu yanatosha, ni mimi Anti Nasra, Shangingi Mstaafu.
0 comments: