Friday, September 5, 2014

KIONGOZI WA AL-SHABABU AUWAWA NA MAJESHI YA MAREKANI.

Kiongozi wa al-Shabab, Ahmed Abdi Godane, aliuawa katika shambulio lililofanywa na Marekani mapema wiki hii, imesema wizara ya ulinzi ya Marekani- Pentagon. Marekani ilifanya mashambulio ya anga Jumatatu usiku na kulenga msafara wa magari ambao kiongozi huyo alikuwa akisafiria. "Kumuondoa Godane kutoka katika uwanja wa mapambano ni hatua kubwa na hasara kwa al-Shabab," imesema taarifa ya msemaji wa Pentagon. Alikuwa mmoja wa watu wanaotafutwa zaidi na Marekani. Donge la dola milioni saba liliwekwa kwa yeyote atakayetoa taarifa za kukamatwa kwake. Pentagon imesema shambulio la kijeshi la Septemba 1 "lilisababisha kifo chake". Marekani imekuwa ikisaidia majeshi ya Umoja wa Afrika kuwaondoa al-Shabab mjini Mogadishu na miji mingine tangu mwaka 2011.

LikeLike · 

0 comments: