Je Unaipenda Facebook ? Mtandao Pinzani Umezinduliwa , Waja kwa Kasi ya Ajabu
Mtandao
wa kijamii wa Ello unapokea maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka
kujiunga kila saa moja hali ambayo inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao
wa Facebook.
Muanzilishi
wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo
unaanzishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.
Mtandao
huu kwa mujibu wa muanzilishi umeanzishwa August mwaka huu ukiwa ambapo
hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama kulipia data.
Hata
hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao
huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.
Baadhi
ya wataalam wa masuala ya kimitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza
gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello
utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.
Paul
Budnitz mtengenezaji wa baiskel za kampuni ya Vermont ameiambia BBC kuwa
wapo imara katika ushindani wa kimitandao na kujigamba kuwa ana
wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzani.
Hata
hivyo kuhusiana na baadhi ya watu kuuita kwa jina la bandia la
anti-Facebook mtandao huo yeye amesema wanajiendesha kama mtandao wenye
mtazamo wake binafsi na si kutegemea mtazamo wa mtandao wa Facebook.
0 comments: