HUKUMU YA OSCAR PISTORIUS YAENDELEA
Oscar
Pistorius akiwa amesimama ndani ya mahakama jijini Pretoria baada
ya Jaji Thokosile Masipa kuwasili kwa ajili ya kusoma hukumu.
Oscar Pistorius akisikiliza hukumu yake.…
Oscar
Pistorius akiwa amesimama ndani ya mahakama jijini Pretoria baada
ya Jaji Thokosile Masipa kuwasili kwa ajili ya kusoma hukumu.
Oscar Pistorius akisikiliza hukumu yake.
Pistorius akiwa amezungukwa na walinzi, polisi, wanahabari na mashabiki wake wakati akiwasili mahakamani.
Kaka
wa Pistorius, Carl Pistorius akiwasili mahakamani akiwa katika baiskeli
baada ya kuumua vibaya katika ajali ya gari mwanzoni mwa mwaka huu.
Mama mzazi wa Reeva Steenkamp, June (wa pili kulia) akiwa na baba wa marehemu Reeva, Barry Steenkamp (kulia) wakati wakiwasili katika Mahakama Kuu jijini Pretoria.
Baba mzazi wa Oscar, Henke Pistorius akiwasili mahakamani.
Jaji Thokozile Masipa akipitia majumuisho ya kesi ya mwanariadha Oscar Pistorius kabla ya kutoa hukumu.
Picha
hii inaonyesha damu zikiwa zimetapakaa chooni kwa Pistorius baada ya
kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp siku ya Wapendanao mwaka
jana. Kulia ni bastora aliyotumia mwanariadha huyo.
HUKUMU ya mwanariadha mwenye ulemavu wa
miguu, Oscar Pistorius wa nchini Afrika Kusini inaendelea kwa sasa
katika Mahakama Kuu jijini Pretoria.
Hukumu hiyo inasomwa na Jaji Thokozile
Masipa ambapo iwapo itabainika kuwa alimuua makusudi mpenzi wake Reeva
Steenkamp anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 25 jela.
Miongoni mwa waliohudhuria hukumu hiyo ni
upande wa marehemu Reeva ambapo yupo mama yake mzazi, June na baba yake
Barry huku upande wa Pistorius akiwepo baba yake Henke Pistorius, kaka
yake Carl Pistorius aliyepata ajali mwanzoni mwa mwaka huu na kuumia
vibaya pamoja na wengineo.
Mapitio ya hukumu hiyo yameanza kusomwa majira ya saa 3: 30 leo asubuhi na bado yanaendelea.
0 comments: