Sunday, September 14, 2014

Dokii Afichua Siri ya Vigogo Kuwakwepa Mastaa wa Kike Bongo, Skendo Chafu zatajwa

UMMY Wencelaus ‘Dokii’ ametoa maneno mazito ambayo wasanii wa kike wanatakiwa kuyasikiliza kwa umakini mkubwa.

Dokii ambaye ni msanii wa kike anayeonekana kuwa karibu na baadhi ya wanasiasa, alisema viongozi wengi wa kubwa wa serikali ya Tanzania wanaogopa kuwa karibu na waigizaji wengi wa kike kutokana na kuandamwa na kashifa kila kukicha.

Msanii huyo aliongeza kuwa yeye anaweza kuwa karibu na vigogo hao kwa kuwa anajiheshimu na kuheshimu sanaa yake.

“Kati ya wasanii wa kike kumi bora wa Tanzania hakuna mwenye uwezo wa kuomba ahadi ya kuonana na mheshimiwa na kukubaliwa huwezi kumpata hata mmoja kwa sababu wamechafuka kwa kashifa,”anasema Dokii.

Dokii anasema kuwa yeye yupo tofauti na wasanii wenzake kwani anatumia umaarufu wake kufanya biashara na si kutumia mwili wake vibaya kitu kinachowaharibia baadhi ya wasanii wa kike wa Bongo movie.

Baada ya kugundua hilo, Dokii anatoa somo kwa wasanii wa kike hususan chipukizi ambao wanataka kujiunga na sanaa waangalie kazi na siyo mapenzi.
                                      www.2todayhabari.blogspot.com

0 comments: