Anashinda Whatsapp Masaa Yote, Ila Nashindwa Kumbwaga
Huyu dada nimemfahamu miaka mitatu iliyopita.
Ni
mwanasheria kwenye firm fulani jijini Dar, nilikuwa nina mpango wa
kumuoa haraka, ila mmoja wa marafiki zake wa karibu aliniambia
nijitahidi kumfahamu kwanza kabla sijaamua kumuoa nadhani alihisi kitu.
Kufahamiana naye kwa muda tukaishia kupata mtoto mmoja wa kike ambaye sasa ana miaka miwili.
Ni
mwanamke mzuri sana, ni gumzo kila anapopita au kufanya kazi, hata
nilitaka nitoane macho na shiny surface mmoja wa firm yake.
Kwa kweli anaita kila jicho ana mengi mazuri, lakini pia ana mapungufu yaliyonipigisha breki kali juu ya tope.
Kwa
sasa anaishi na wazazi wake, lakini mara nyingi saba tunalala kwangu.
Nafahamika kwao kama mzazi mwenza, kwetu pia kaskazini wanamtambua.
Amekuwa
ni mwepesi sana wa kupata marafiki wa kiume, ana hasira za karibu,
kujiachiachia sana kwa wanaume imekuwa sehemu ya maisha yake, yeye
anadai si wapenzi wake. Wanataniana tu hii ni moja ya sababu iliyonizuia
kumuoa.
Nilihisi
kama hajiheshimu.hayuko tayari kuishi kama mke wa mtu nikadhani
nimwache kwanza ale maisha wakati nami nakula taratibu ingawa nahofu ya
magonjwa.
Simu zake sijawahi ziona hata mara moja zikiita kwa sauti toka nimfahamu.anashinda watsapp 24/7.
Facebook
kwake ni kama oxgen, kila siku anaongeza wanaume, viber anatumiwa mioyo
na mikisi ya wanaume, linkedin pia hayuko mbali.
Nahisi
kweli atakuwa ananipenda, lakini kwa hayo nashindwa kuji commit, ila
bahati mbaya nashindwa hata kumuacha, hasa ukizingatia nina mtoto naye.
Yaani sijui nifanyeje, nimbwage.
Naona sio waifu matirio.
Ataniua jamani.
0 comments: