Phiri amkubali Okwi shingo upande
Na Wilbert Molandi, Unguja
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Phiri, ameshtushwa na usajili wa kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi aliyetua kuichezea timu hiyo.Simba, juzi Alhamisi, ilitangaza kumrejesha kundini kiungo huyo mwenye mkataba wa mwaka miwili wa kuichezea Yanga inayojiandaa na Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Phiri raia wa Zambia, alisema hajui lolote kuhusu usajili huo na kusisitiza…
Na Wilbert Molandi, Unguja
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Phiri, ameshtushwa na usajili wa kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi aliyetua kuichezea timu hiyo.Simba, juzi Alhamisi, ilitangaza kumrejesha kundini kiungo huyo mwenye mkataba wa mwaka miwili wa kuichezea Yanga inayojiandaa na Ligi Kuu Bara msimu ujao.
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Phiri, ameshtushwa na usajili wa kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi aliyetua kuichezea timu hiyo.Simba, juzi Alhamisi, ilitangaza kumrejesha kundini kiungo huyo mwenye mkataba wa mwaka miwili wa kuichezea Yanga inayojiandaa na Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Phiri raia wa Zambia, alisema hajui lolote kuhusu usajili huo na kusisitiza kuwa hakushirikishwa kwa kuwa alijua tayari anao wachezaji watano wa kimataifa kama sheria za za soka zinavyotaka.
“Sijui chochote, lakini kama wamemsajili nafikiri ni jambo zuri na mimi nipo tayari kufanya naye kazi, “Mimi kama wewe tu ndugu mwandishi, sijui lolote kuhusiana na usajili wa Okwi, mimi nimesikia tu kuwa Okwi amesaini Simba.“Sasa nashindwa kuelewa amesaini vipi Simba wakati ni mchezaji mwenye mkataba wa kuichezea Yanga, ngoja nisubirie taarifa rasmi kutoka kwa viongozi.
“Ngoja tuone kwa sababu soka la Tanzania lina mambo mengi, itatubidi tumkate mchezaji mmoja, kwa taarifa nilizozipata (Donald) Musoti anatakiwa kukatwa na badala yake (Juma) Nyosso arejee.“Lakini hata kama Nyosso akisaini Simba, bado Musoti nilikuwa namhitaji, kiukweli hauwezi kumhukumu mchezaji kwa mechi mbili ambazo amezicheza za kirafiki hapa Zanzibar,” alisema Phiri.
0 comments: