PAPA KUJITABIRIA KIFO,WAUMINI WAANZA MAJONZI
MAJONZI:yameanza baadhi ya waumini wa kanisa katoliki bongo,kufuatia kiongozi wa dunia PAPA
(77)kuweka hadharani hatma ya maisha yake.Katikati ya wiki hii papa francis akiwa anarejea vatcani kutoka
ziaran korea kusini alisema anaamini ana miaka miwili au mitatu ya kuishi duniani na si vinginevyo,,najaribu kufikiria vizuri zambi zangu na makosa yangu siwezi kujivuna kwa sababu najua hali hii itadumu kwa muda mchache.miaka miwili au mitatu nitakua nimeondoka na kwenda nyumbani kwa baba,,Alisema papa huyokauli iliyo zua sintofahamu duniani.
Wachambuzi wa maswala ya kiimani kwa nyakati tofauti,huenda kiongozi huyo anatatizo la kiafya ambalo halijawekwa wazi.Jijini dar-er-salam baadhi ya waumini wa kanisa katoliki waliozungumza na gazeti hili walisema kauli hiyo ya papa iliwatia majonzi kwani inawapa tafsiri ya kumkosa sikunyingi.
Samuel msokani anaabudu katika kanisa katoliki parokia ya mtakatifu maximillian kolbe,mwenge yeye alisema,.Nimepokea kwa majonzi makubwa,kauli ile ya papa kama anaumwa atuweke wazi waumini wake.
Kama amepewa maono na mungu pia atuweke wazi waumini wake tujue.Mama juliana yeye anaabudu katika kanisa katoliki la mtakatifu joseph jimbo kuu katoliki daresalam alisema,siamini kama kweli papa alisema yale maneno ni makali sana na yanachoma nilitoa machozi niliposikia nilianza kulia hata kabla ya sikuyake haijafika.Muumini mwingine anaye abudu katika kanisa katoliki parokia ya mtakatifu anuarite,makuburi(aliomba jinalake lisiandikwe),Alisema anaamini kuwa papa atakua ameona katika maono ya kifo chake kwasababu ya usafi wa moyo wake,,mimi na amini papa ni msafi wa moyo kwahiyo ameonyeshwa na mungu kwamba muda wake wa kumtumikia duniani umeisha kule kusema ni kutuweka tayari kupokea taarifa.Alisema muumini wa kiume
0 comments: