Utata Watawala Taarifa za Kuuawa Kiongozi wa Boko Haram
Taarifa zilizosambazwa na baadhi ya
vyombo vya habari nchini Nigeria zinadai kuwa kiongozi wa kundi la
kigaidi la Boko Haram, Abubakar Shekau ameuwa na majeshi ya Nigeria.
Tetesi hizo zilianza kusambaa Alhamisi
iliyopita baada ya jeshi la Nigeria kutoa taarifa kupitia Twitter kuwa
wamemjeruhi vibaya kiongozi wa ngazi za juu wa Boko Haram katika eneo la
Konduga, Borno.
Wikendi iliyopita taarifa hizo zilianza
kuaminika zaidi baada ya picha zinazoonesha mwili wa mtu anaeaminika
kuwa Abubakar Shekau kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na tovuti
mbalimbali.
Hata hivyo, msemaji wa jeshi la Nigeria
amekataa kuthibitisha taarifa hizo wala kuzikanusha akidai kuwa bado
uchunguzi unaendelea.
“Katika point hii, sitaweza
kuthibitisha au kukanusha taarifa hizi. Major General Chris Olukolade
(Msemaji wa jeshi la Ulinzi) ataweza kutoa taarifa kuhusu hali hiyo hivi
punde. Endeleeni kusubiri.” Msemaji wa jeshi la Nigeria, General
Olajide Olaleye aliiambia AFP jana.
Jeshi la Nigeria linapata kigugumizi
kuhusu taarifa hizo kwa kuwa miaka iliyopita waliwahi kutangaza kumuua
Shekau na baadae akatokea na kutangaza uwepo wake kupitia kipande cha
video.
July 30, 2009, kitengo cha ulinzi cha
jiji la Maiduguri walieleza kuwa wamemuua Abubakar Shekau aliyekuwa
msaidizi wa mwanzilishi wa Boko Haram, Mohammed Yusuf katika shambulizi
lililosababisha vifo vya wapiganaji 200 wa kundi hilo.
Lakini kabla mwaka haujaisha, Shekau alijitokeza kupitia kipande cha video na kukanusha taarifa hizo.
June 30 mwaka jana, vyombo vya usalama
vilieleza kuwa Abubakar Shekau anahofiwa kufa katika mapigano makali
yaliyotokea kaskazini mwa Nigeria.
Wiki kadhaa baadae alijitokeza tena na kukanusha habari hizo kupiti mkanda wa video.
“Here is Shekau, Shekau, Shekau, Shekau, original… I want the total world to know that I’m alive by the grace of Alla.”
0 comments: