Ajabu: Anamkodisha Mpenzi wake kwa Yeyote Apate Pesa ya Kununua iPhone 6
Mwanafunzi wa Chuo kikuu kimoja cha
China ambaye jina lake halikutambulika kwa haraka ameamua kufanya
‘uchizi’ ili mradi tu aipate pesa ya kununua aina mpya ya iPhone
iliyoingia sokoni, iPhone6.
Kijana huyo alionekana akiwa nje ya
chuo kikuu cha Songijiang akiwa na bango kubwa lililoandikwa kwa kichina
na kutafsiriwa ‘Girlfriend Sharing’.
Katika tangazo hilo kijana huyo
anaeleza kuwa yuko tayari kumkodisha mpenzi wake kwa mtu yeyote
atakayeweza kutoa pesa ili jamaa apate kiasi cha kutosha kuinunua iPhone
6 yenye screen kubwa.
Picha ya kijana huyo imesambaa kwa kasi katika mtandao wa kijamii unaotumiwa na wachina uitwao ‘Weibo’ ambao ni kama Twitter.
Tangazo hilo limeambatana na picha za
mpenzi wake na amewatoa hofu wateja wanaosita kuingia nae mkataba kuwa
hata mpenzi wake ameridhia na yuko tayari kudate na mtu yeyote
atakaejitokeza.
Muda wa kuwa na msichana huyo baada ya
kumkodi umebainishwa kutokana na malipo yatakayofanywa na mteja. Viwango
ni vya saa 1 (10 yuan), siku 1 (50 yuan) au mwezi mmoja (500 yuan).
Hata hivyo, wapenzi hawa sio wa kwanza
kujiweka sokoni ili wapate bidhaa ya kampuni ya Apple. Mwaka jana katika
uzinduzi wa iPhone 5, wanandoa wa Shaghai waliwaweka sokoni watoto wao
watatu ili wapate pesa ya kununua computer na simu za iphones lakini
walikamatwa na kufunguliwa mashitaka.
Lakini pia kijana mdogo wa Hunan alijitolea kuuza figo lake ili apate pesa ya kununua iPad na iPhone.
Siyo hayo tu, hivi karibuni mwanaume
mmoja wa Saudi Arabia ametaka kupewa iPhone 6 kama mahari ya dada yake
hata kabla aina hiyo ya simu haijazinduliwa Bahrain.
0 comments: