Saturday, September 13, 2014

OBAMA AONYA KUHUSU MKWAMO WA BAJETI











 Washington. Rais wa Marekani, Barack Obama amewataka wabunge wa Chama cha Republican waache vitisho na wapitishe bajeti ili kukomesha kufungwa kwa shughuli za Serikali.
Ombi hilo la Obama limekuja wakati baadhi ya wafanyakazi wa Mpango wa Huduma ya Bima ya Taifa ya Afya wakiendelea kulalamika kwamba huduma hizo zitaendelea kukabiliwa na matatizo kwa miezi kadhaa ijayo, kutokana na kutokuwepo kwa huduma za tovuti ya mpango huo.
Katika hotuba yake iliyoonyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni, Obama ameonya kushindwa kwa Marekani kulipa madeni yake huenda kukasababisha athari na kuwahimiza wabunge wa Chama cha Republican kuongeza bila masharti kiwango cha fedha ambazo taifa linaweza kukopa.
Rais Obama amewaambia waandishi wa habari kwamba hakuna anayepaswa kuzuiliwa mateka katika kutekeleza mpango huo muhimu kwa raia wote wa Marekani bila kujali itikadi za vyama vyao.
Obama pia alisema kama Bunge litakataa kukiongeza kiwango hicho, Marekani haitaweza kugharimia shughuli zake zote kifedha kufikia katikati ya mwezi huu.
                                    www.2dayhabari.blogspot.com

0 comments: