Saturday, September 13, 2014

MIAKA 18 YA KIFO CHA TUPCA WASANII MMEJIFUNZA NINI?


Tupac Amaru Shakur 
Kwa ufupi
Anaitwa Tupac Amaru Shakur, mwanahipop aliyefariki dunia akiwa na umri mdogo wa miaka 25 ambaye mpaka leo bado dunia inamkumbuka, na mashairi yake yakitumika katika vyuo mbalimbali kufundisha falsafa ya kisasa, huku wengine wakimtumia kama mfano wa kuigwa kutokana na mashairi yake ya kupinga ubaguzi na kuburudisha wakati mwingine.
SharLeo dunia nzima inaadhimisha miaka 18 ya kifo cha nguli wa muziki wa kizazi kipya aliyewahi kuitikisa dunia ya vijana kwa miaka isiyozidi minane akiwa kinara na kisha kuaga dunia kwa kupigwa risasi na mahasimu wake na kufariki dunia siku ya saba baada ya kupoteza damu nyingi.
Anaitwa Tupac Amaru Shakur, mwanahipop aliyefariki dunia akiwa na umri mdogo wa miaka 25 ambaye mpaka leo bado dunia inamkumbuka, na mashairi yake yakitumika katika vyuo mbalimbali kufundisha falsafa ya kisasa, huku wengine wakimtumia kama mfano wa kuigwa kutokana na mashairi yake ya kupinga ubaguzi na kuburudisha wakati mwingine.
Ukiachana na ukorofi wake na mambo mbalimbali ambayo hayakupendeza kwa jamii bado dunia inamlilia kwa jinsi alivyoweza kuleta changamoto na mwamko kwenye muziki huo wa kizazi kipya, mpaka ukapata umaarufu mkubwa duniani.
Hapa ndipo kiuhalisia tunapata mshangao kwamba mara nyingi mtu huyu alikuwa mkorofi mkorofi, lakini leo dunia ya sanaa inasimama dakika moja na kumkumbuka kwa jema moja tu, changamoto katika muziki wa kizazi kipya.
Baada ya kuliona hilo tunarudi tena kwenye tasnia yetu ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini, sijui wana Hip Pop wetu wamejifunza nini na wao siku wakiondoka tutajifunza nini kutokana na sanaa yao?
Wasanii wetu, kwa kweli bado ni watu ambao wenyewe kama walivyo hawana ile nguvu ya kuamua jambo kwa mmoja, mmoja kwa manufaa ya wengi au kuanzisha msukumo fulani ambao kila mtu akiuona atatamani kuwa kama yeye, ni wachache sana.
Sasa hivi ukiuliza msanii aliyejiweka kwenye nafasi nzuri utatajiwa AY aliyejianzishia miradi mingi ambayo kila mtu anatamani kuwa kama yeye, huku akiamini ameanzisha bila kujihusisha na kashfa, yoyote na ameweza kupenya kwenye mipaka ya nchi mbalimbali kufikisha muziki wake.
Wanaharakati walikuwepo lakini baada ya kufanikiwa kwa jitihada binafsi, harakati wameziweka pembeni na kuwaacha wa chini ambao walikuwa wakiendelea kutaabika mpaka wengine wameamua kujishusha na kuomba misamaha kwa wale waliokuwa wakiwashutumu kuwaonea.
Hii ni alama tosha inayotuthibitishia kwamba bado wasanii wa nyumbani wana safari ndefu kisanii na kimafanikio, na sababu kubwa ya msingi inayokwamisha maendeleo yao yote hayo ya aina mbili ni kutokana na kutotambua hasa wanataka nini.
Wasanii wetu wamekosa misimamo katika viwango vya kazi zao kuanzia kwenye kulipwa mpaka kwenye utengenezwaji wake. Utakuta wasanii wawili wanafanya muziki wa aina moja, lakini huyu analipwa 10, huyu analipwa tano na maisha yanaenda.
Mpaka leo wasanii wetu wanaweza kutishwa na kituo kimoja cha redio kwa kuambiwa ‘hatupigi nyimbo zenu’ na wakaogopa kiasi cha kupiga magoti huku wakijua dhahiri kwamba ili kituo kifanye kazi zake kwa ufanisi kinahitaji nyimbo za wasanii.
Kuna kitu cha kujifunza sasa kwa Tupac ambacho tungetamani wasanii wetu wakijue kinaitwa misimamo, waepukwe kuendeshwa kama magari mabovu, wawe na uamuzi wao ili kesho na keshokutwa, kuwe na msingi kwa ajili ya wasanii wanaokuja.
                                                     www.2dayhabari.blogspot.com

0 comments: