Ni muda mfupi uliopita jopo la majaji
wa mahakama ya Afrika mashariki huko Arusha imetoa uamuzi wa Shauri
ambalo ilifunguliwa na CHADEMA ( Antony Komu ) aliyekuwa mgombea wa
Chadema katika Bunge la Afrika mashariki , ambaye alifungua kesi ya
msingi kuhusu kukiukwa kwa hati ya makubaliano ya Afrika ya mashariki ,
kutokana na Chadema kutokupata nafasi wakati hati iko wazi na imeelezea
kinagaubaga jinsi ya kupata wawakilishi kutokana na uwiano wa vyama
katika mabunge ya nchi washirika .
mahakama
ya Afrika mashariki , imesema kuwa Bunge na serikali walikiuka hati
hiyo ibara ya 50 , na pia kitendo cha kumpa fursa kugombea John Lifa
Chipaka wakati chama chake hakina mbunge ni muendelezo wa kukiukwa kwa
hati hiyo ya Afrika mashariki .
Jopo
la Mawakili wa Chadema lilikuwa likiongozwa na Edson Mbogoro , Aidha
mahakama imeitaka serikali kulipa Antony Komu gharama zote za kesi .
Huu
ni muendelezo wa CCM kujidhalilisha kwa kutumia mabavu kwani
mliofuatilia mtakumbuka kuwa kulikuwa na ubishani mkubwa sana wa
kikanuni ndani ya Bunge siku ya uchaguzi huo, hukumu hii itasaidia sasa
ile kesi ya pili ambayo iko mahakama kuu Dodoma ya kuitaka mahakama hiyo
itengenezwe uchaguzi ule na irudi we upya kuendelea kwa kasi .

No comments:
Post a Comment