Kajala Masanja amedai kuwa maisha yake hayajabadilika sana kama ambavyo magazeti ya udaku yamekuwa yakiandika.
Muigizaji huyo wa filamu alisema
kuwa tetesi kuwa ana fedha nyingi kiasi cha kuwa na mpango wa kumwajiri
Wema Sepetu ni uzushi mtupu. “Mbona maisha yangu ni ya kawaida sana,”
Kajala aliiambia Bongo5.
“Mimi naona nipo vilevile hakuna
kubwa sana lililongezeka. Nafanya shughuli zangu tu. Tatizo watu
wanaamini sana magazeti. Mimi sina utajiri huo wanaouzungumzia, Kajala
ni yule yule,” alisisitiza.
Hivi karibuni Kajala alizindua filamu yake fupi iitwayo ‘Mbwa Mwitu’.

No comments:
Post a Comment