Monday, September 29, 2014

Ndoa ni DIRECT VISA To Hell Kama Ukiichukulia Poa, Ni Heri Usioe ama Kuolewa Kama Humaanishi

Kila mtu anataka Kuolewa lakini shida ni Vigezo vya Waoaji vikoje??Kila siku vigezo vinabadilika..Sasa hivi unaangaliwa sana uwezo wako wa mfukoni kabla hujaambiwa NDIO…Hela imekuwa ndo GREEN LIGHT,ukiwa hohehahe basi utazungushwa wee na utaambiwa kila siku,”IAM NOT READY FOR MARRIAGE”
Kuna watu wametoswa kisa Wallet hazisomi na ukashangaa wameolewa na watu kisa WANA HELA..
Hela ingekuwa kila kitu AMBER ROSE na WIZ KHALIFA wasingeachana..Wana kila kitu wale…
Hela ingekuwa jawabu NICK CANNON na MARIAH CAREY wasingeachana…
Hela ingekuwa kila kitu JASON DERULLO na JORDIN SPARKS wangekuwa happily married lakini Wapi…
Raha ya ndoa itoke Moyoni…Mpendane kwa jinsi mlivyo…Mpendane kwa hali yoyote mliyonayo na muelewane..
Kuna watu kula kwao ni kwa mbinde lakini ndoa yao ina amani na furaha mwaka wa 20 huu…Kuna watu wana kila kitu,Magari,Mashamba,Viwanja,Akaunti zilizonona lakini hata miaka 3 wameshindwa kufikisha…Wamekuwa WATALAKA VIJANA…
Ndoa ni DIRECT VISA to Hell kama ukiichukulia poa,ni heri Usioe ama kuolewa kama humaanishi…Maana ukiachana na mwenza wako ndani ya miaka 3 hiyo miaka mingine yoooteee UNAZINI TU…Mbingu utaisikia kwenye kipindi cha JAHAZI tu…
Jifunze kwa Wajane na Watalaka…Jua unachotamani na UJIPANGE!

0 comments: