MAXIMO ANATUELE`ZA HATUNA MSHAMBULIAJI WA AINA HIO
Wengi
tulivyokuwa hatuna aibu hata ya kushngaa tutaanza kumsifia mchezaji
mpya wa Daraja la Chini kule Brazil Genilson Santana Santos ‘Jaja’
ambae leo amejichotea sita za bure mbele ya kocha Mbrazil, Marcio
Maximo baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 kwenye mechi
ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Binafsi
nimemtazama mara kadhaa katika mazoezi ya yanga paleLoyola la msingi ni
kuwa Kocha Marcio maximo Tangu akiwa katika timu ya taifa ya Tanzania
leo amewatukana Rasmi watanzania tena kisomi kwa kuwaeleza kuwa Hatuna
mshambuliaji .
Binafsi
ukimtazama Jaja ni mchezaji mbaye ana umbo kubwa mwenye mwili mzito
kidogo lakini mwingi wa akili ukitazama goli la kwanza na la pili jaja
amezoea kufunga tangu akiwa kwao Brazil .
Marcio
alivyokuwa Timu ya taifa ya Tanzania alikuwa mara kadhaa akitafuta
washambuliaji na wamepita wengi lakini leo ameaumua kuwaeleza ukweli
kuwa hakukuawa na mshambuliaji katika timu ya taifa ya Tanzania
Binafsi
nimeanza kuiona yanga ambao sikuwa kuiona kabisa kwa miaka mingi
fizikia ,umakini wa viungo uimara wa safu ya ulinzi wakati fulani tuwe
tunashawishika kuangaalia Sayansi ya soka inakwendaje lakini sio kupiga
zogo tu ohooo yanga ,yanga simba ,simba, Azam kiboko yao swala kubwa
wachezaji na uwelewa kwa walimu nadhani leo marcio maximo katufundisha
jinsi ya kuwa na mshambuliaji anayejua kufunga .
Si
ajabu watu wataanza kukumbuka na kuanza kusema arejeshwe kwenye timu ya
taifa ndio tulivyo sisi tuna ulimbukeni wa hali ya juu kweli ni kipi
hasa tulichomwondolea Maximo leo anakuja kukifanya katika ardhi ya
Tanzania tena kwenye timu yetu ya kizalendo sasa shida nini ?
Hatuna
wafungaji magoli tunawabahatisha magoli kwa miaka miwili iliyopita
mfungaji bora katika nchi nyingine kwenye ligi yetu hii ni aibu tosha
Leo
kule kwenye magazeti ya Kireno Brazil watashangaa kuona kijana
asiyejulikana katika fukwe za kopa capaba anaonekana Dhahabu hapa ndipo
tunapoonyesha kiwango chetu cha juu cha ujinga tulinao ambao maximo
katufundisha hakuna mafanikio ya Haraka katika soka .
|
0 comments: