Ali Kiba Atoa ya Moyoni ‘Lulu Michael Anafaa Kuwa Mke’
Stori: Erick Evarist na Sifael Paul
HII ni
exclusive! Kwa mara ya kwanza, staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo
wake wa Mwana, Ali Kiba amefunguka kuwa mwigizaji kiwango Bongo,
Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anafaa kuwa mke (wife material) huku
akiweka wazi sifa kibao alizonazo, Wikienda liko bize kukujuza.
Kiba
ambaye hivi karibuni ameibua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii,
usafiri wa umma na kwenye baa juu ya ujio wake mpya akisemekana kurudia
kiti chake ambacho alikikalia Mbongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ kwa
muda, mwaka 2010 aliwahi kuripotiwa katika magazeti pendwa kwamba ana
uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye wakati huo alikuwa na umri chini ya
miaka 18!
LULU ANAFAA KUWA MKE
Akizungumza
mbele ya kinasa sauti cha Globa TV Online, Bamaga-Mwenge jijini Dar
mwishoni mwa wiki iliyopita, Kiba ambaye anatarajia kuangusha shoo ya
kihistoria Agosti 8, mwaka huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, alisema Lulu anafaa kuwa mke kwa vile
ni mchapakazi sifa ambayo mke mwema anapaswa kuwa nayo.
AMMWAGIA SIFA
Kiba
alisema Lulu anajua kuhangaika, anajua kupambana kusaka pato lake
kihalali kupitia mauzo ya sinema zake anazozizalisha kitu ambacho
kinawashinda mabinti wengi na kuangukia katika biashara ya kuuza miili
(ukahaba).
Licha
ya kummwagia sifa hizo, kipindi hicho alichokuwa akitajwa kuwa naye,
Lulu alikuwa na matukio ambayo hayakuwa na maadili lakini Kiba hayo
hakuyatilia maanani.
Mwandishi: Unafikiri Lulu ni ‘wife material’ (mke mwema) ambaye unaweza kumweka ndani akalea watoto na kuijenga familia bora?
Kiba: Yeah! Anafaa kuwa mke, ni binti anayejituma, mchapakazi, mtafutaji. Kwangu mimi mtu wa namna hiyo ndiyo anafaa kuwa mke.
Mwandishi: So, unataka kutuambia kwamba unaweza kumuoa?
Kiba: Sijasema hivyo mimi, nimesema anafaa kuwa mke.
ACHOMOA KUBANWA KISHERIA
Licha
ya kuchomoa ishu hiyo ya uhusiano, mapaparazi wetu walimbana zaidi staa
huyo afafanue kwa nini alitajwa yeye na si msanii mwingine huku ikidaiwa
kuwa, Lulu hakuwa ametimiza miaka 18 hivyo kubanwa kisheria (ya watoto
na kujamiiana).
“Sijatembea
naye ndiyo maana unaona hata sheria haijanihukumu, endapo ningekuwa
nimetembea naye, basi sheria ingeweza kunitia hatiani na ningefungwa
jela,” alifafanua Kiba.
AWASHANGAA WANAOMSHANGAA
Kiba aliongeza kuwa, anashangaa sana kuona watu wanamsema vibaya yeye kupendwa na Lulu.
“Lulu
ni msanii mwenzangu, anapenda kazi zangu na mimi napenda za kwake. Ni
rafiki wa kawaida, hakuna kitu kingine cha ziada. Nawashangaa wanaozusha
ya kuzusha, hivi kwani kuna tatizo Lulu akinipenda? Sidhani kama ni
kosa, ana haki ya kunipenda kutokana na muziki wangu.
“Unajua
muziki mzuri huwa unapenya automatically, huwezi kuzuia hisia za
muziki, mtu unaweza ukawa humpendi msanii f’lani lakini ukapenda muziki
wake, unajikuta tu unampenda, unaanza kuimba nyimbo zake,” alisema Kiba.
KUMBUKUMBU MBICHI
Juzikati
wakati Kiba anatambulisha nyimbo zake mbili kwa mpigo (Mwana na
Kimasomaso), Lulu, kupitia mtandao wa Instagram alitupia maneno ya
kummwagia sifa staa huyo, liliibuka kundi ambalo linatajwa kuwa ni
wafuasi wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Team Wema’ na kuanza kumshambulia kwa
maneno machafu.
KIBA AFUNGUKA
Akizungumzia
ishu hiyo, Kiba alisema waliofanya hivyo hawakumtendea haki Lulu kwani
ana haki ya kueleza hisia zake pale anapoguswa na muziki mzuri.
“Hawajatenda haki kwa sababu Lulu ni binadamu kama walivyo wengine, ana haki ya kupenda kitu kizuri,” alisema Kiba.
KUHUSU KIFO CHA KANUMBA
Kiba
akizungumzia juu ya kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa nyota wa sinema
Bongo, marehemu Steven Kanumba ambapo alidaiwa kunaswa kwa meseji za
mapenzi alizozituma kwa Lulu ndiyo zilizosababisha mtifuano ambao
ulisababisha kifo cha Kanumba, alikana madai hayo.
“Si
kweli, sikuwa nimewasiliana na Lulu siku hiyo kabla ya tukio. Nakumbuka
nilikuwa safarini, baada ya tukio nilimpigia Lulu kutaka kujua ukweli wa
taarifa za kifo kwa sababu marehemu alikuwa mtu wangu wa karibu kama
alivyo Lulu,” alisema Kiba.
AMGUSIA WOLPER
Kwenye
mahojiano hayo, mkali huyo alizungumzia ishu ya mwigizaji, Jacqueline
Wolper kukiri kwamba Kiba ndiye mwanaume aliyemtoa usichana wake kwenye
simulizi iliyochapishwa katika Gazeti la Championi hivi karibuni.
“Mh!
Aliwahi kukiri? Daah! Sijui bwana… Wolper ni mtu wangu wa karibu kama
alivyo Lulu,” alisema kwa mkato Kiba.Juzi, Lulu alitafutwa na mapaparazi
wetu ili azungumzie ukaribu wake na Kiba, lakini simu yake muda mwingi
iliita bila kupokelewa (tunaamini atasoma hapa, tunaendelea kumtafuta
ili afunguke).
www.2dayhabari.blogspot.com
0 comments: