Thursday, November 13, 2014

MATUSI YA MITANDAONI BADO NI TATIZO NCHINI



Salma Omar Yusuf anayedaiwa kumtusi Nadya.
SUALA la matumizi ya mitandao ya kijamii katika kujielimisha, kuhabarika na kuburudika kwa sasa limegeuka na kuwa uwanja wa kutupiana matusi.

Nadya Masoud Mohammed mlalamikaji.
Kwa sasa watumiaji wamebadilika na kutumia mitandao ya kijamii katika kuharibu maadili ya jamii hasa ya Waafrika na kusahau malengo makuu ya kuanzishwa kwa mitandao hiyo.
Mbali na taasisi mbalimbali kukemea matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, bado jamii yetu inaonekana kuendelea kutumia mitandao ndivyo sivyo.

Sehemu ya matusi aliyoyatoa Shamah kwa Nadya.
Juzi katika mkutano wa wamiliki wa mitandao ya kijamii hususan 'Blogs' uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma aliwaasa wamiliki hao kuitumia vizuri mitandao ya kijamii ili kulinda maadili ya Mtanzania.
Katika tukio la hivi karibuni ambalo limeacha mshangao kwa baadhi ya watumiaji wa Mtandao wa Kijamii wa Facebook, ni matusi ya nguoni yaliyotolewa na mwanadada Salma Omar Yusuf ‘Shamah’ kwa mwenzake Nadya Masoud Mohammed.

Muendelezo wa matusi aliyoyatoa Shamah.
Wanadada hao wote ni wakazi wa Zanzibar ambapo inadaiwa kuwa Shamah ni mtoto wa waziri mmoja kisiwani humo na katika Mtandao wa Facebook anatumia jina la ‘Shamah Yussuf’.
Katika kuonyesha kuwa matumizi ya mitandao kwa sasa yamebadilika, Shamah alifikia hatua ya kutumia maneno makali yasiyofaa kutumika mbele ya jamii wakati akimshambulia kwa matusi mwenzake.
Baada ya Shamah kuona anashambuliwa vikali na baadhi ya wasomaji kwa matusi hayo, aliamua kuondoa ujumbe uliokuwa na matusi japo alikuwa tayari amechelewa na ulikuwa tayari umenakiliwa.
Kufuatia matusi hayo, mwanadada huyo amefunguliwa kesi ya matusi na kumtishia kummwagia tindikali mwenzake yenye jalada namba MAZ/RB09/2014 katika Kituo cha Polisi Mazizini.

RB ya kesi aliyofungua Nadya dhidi ya Shamah.
Mtandao huu ulimtafuta mlalamikaji ambaye ni Nadya ambaye alisema hana ugomvi wowote na mwanadada huyo na wala hamfahamu jambo linalomfanya ashangae kwa nini amtishie kumwagiwa tindikali hali iliyomfanya aende katika kituo cha polisi kutoa taarifa.
Mtandao huu ulipoongea na mtuhumiwa Shamah yeye alisema kuwa hajawahi kumtukana wala kumtishia kummwagia tindikali Nadya.
Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Zanzibar kuzungumzia tukio hilo bado zinaendelea.

0 comments: