Ni rahisi sana Sana Kwa Mwanandoa Aliyeajiriwa Hapa Mjini Kuchepuka, Hivi Ndivyo Wanavyofanya
Nina
uzoefu kidogo na mambo ya kazi za ajira maofisini, nimefanya hivi kwa
muda mrefu. Wakati flani nilifanya kazi katika ofisi zilizo katikati ya
jiji, kule mitaa ya Posta jijini Dar es Salaam.
Ofisi
nyingi za serikali na watu binafsi zinapatikana mitaa ile. Kutokana na
sababu hiyo, kuna idadi kubwa pia ya migahawa, hoteli, mama ntilie, pub
na kadhalika.
Kuna
mambo mawili makubwa yenye ushawishi mkubwa wa usaliti. Ofa za chakula
au vinywaji na usafiri. Kwa kawaida, wafanyakazi wa ofisi moja hupenda
kutoka pamoja wakati wa chakula cha mchana, wenyewe tunapendelea zaidi
kusema lunch!
Kila
mmoja ana sehemu yake anayokula kulingana na kipato chake, wapo
wanaokwenda Southern Sun kupata chakula cha mchana, na wapo wanaowafuata
mama ntilie wanaojibanza kwenye vichochoro vingi vilivyopo mjini.
Huko
ndiko tunakokutana na akina dada waliovalia vizuri na kupendeza,
wakitokea katika maofisi mbalimbali, huwezi kujua yupi ni mhudumu wa
chai, yupi ni bosi, wote wanang’ara. Na hapa ndipo ofa za misosi
zinapoanza kushawishi ngono.
Kijana
mmoja mwenye kipato kikubwa ofisini kwake, atavutiwa na msichana mrembo
mwenye mshahara wa wastani. Ili kumsogeza karibu, atalipia chakula cha
siku hiyo na kumualika kwa kesho yake. Kulipiwa chakula ni jambo dogo,
lakini lenye thamani kubwa sana. Si rahisi mtu aliyekulipia chakula kwa
nia njema, ukaacha kumshukuru na hata kumwelekeza unapofanya kazi.
“Mimi
nipo pale Oj Traders,” msichana anaweza kujita mbulisha jina na kusema
anapofanyia kazi huku mkaka akimweleza kuwa yeye ni mhasibu katika ofisi
flani. Watakapo
kutana mara ya pili, wataachiana namba za simu.
Baada ya hapo, mkaka atafanya mbwembwe za kuhamahama maeneo ya lunch ili mradi tu mdada wa watu aingie kwenye laini.
Ukimaliza
suala la lunch, kuna hii kitu foleni, hasa kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Raha ya kufanya kazi katikati ya jiji inaingia shubiri kadiri jioni
inavyozidi kusogea. Kuanzia saa kumi, ni vurugu katika vituo vya
daladala na hasa wakati kama huu ambao bodaboda zimezuiliwa kuingia
mjini.
Wenye
magari binafsi ndiyo wakati wao wa kujidai, ingawa foleni inawakumba
wote. Lakini ni afadhali ukiwa kwenye foleni ndani ya gari dogo, mko
wawili kuliko foleni, umeshika bomba kwenye daladala.
Siyo
rahisi kwa mdada kukataa lifti ya kijana mwenye gari. Na katika foleni
ndefu, ni wazi kwamba hadi mwisho wa safari, watakuwa wameshabadilishana
namba. Kwa msichana, kuwa na uhakika wa usafiri kila siku ni ukombozi.
Tusidanganyane,
hakuna msichana ambaye hatajua kuwa lunch au usafiri anaopewa unahitaji
malipo maalum, ambayo ni penzi. Hali hii haiko Dar tu, bali nchi nzima
na pengine duniani kote.
Mwanamke
aliyeajiriwa anakuwa katika mitihani mikubwa zaidi ya kusaliti ndoa au
uhusiano wake, kwa sababu hata kama haitakuwa kwenye chakula au usafiri,
bado watu anaokutana nao katika utendaji wake, wanaweza kumghasi.
Fikiria anakutana na mabosi, marafiki wa mabosi wake, wafanya biashara,
atapona kweli?
Hata hivyo, simaanishi kama tabia hii inawakumba waajiriwa wote, isipokuwa nadhani ni sehemu kubwa wanahusika!
By Mike Tee
0 comments: