Saturday, September 20, 2014

YANGA SC YAPIGWA 2-0 JAJA AKOSA PENALTI MOROGORO


Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar kilichoanza dhidi ya Yanga SC leo katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na kushinda mechi ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara.Kikosi cha timu ya Yanga SC kilichoanza dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakishangilia wakati wa mchezo.
Kipa wa Mtibwa Sugar, Saidi Mohames (18) akiokoa moja ya shambulizi la Yanga SC.
YANGA SC imeanza kwa kipigo cha mabao 2-0 Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutoka Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro mshambuliaji Genilson Santana ‘Jaja’ akikosa penalti.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa, Dominick Nyamisana wa Dodoma, aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Milambo Tshikungu wa Mbeya, hadi mapumziko tayari Mtibwa Sugar walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na Mussa Hassan Mgosi dakika ya 16 aliyemalizia pasi ya kichwa ya Ame Ali na kumuwahi kipa Deo Munishi ‘Dida’ aliyetokea vizuri kutaka kudaka.
Mfungaji wa bao la pili la Mtibwa Sugar ni Ame Ali dakika ya 82 kipindi cha pili.
Yanga SC: Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Omega Seme, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite/Said Bahanuzi dk72, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza/Simon Msuva dk46

0 comments: