Tuesday, September 23, 2014

WAMAREKANI WAFUNGA NDOA KATIKA MLIMA KILIMANJARO


 Kara Lee akimlisha keki mumewe Richard Miller mara baada ya kufunga ndoa katika Mlima Kilimanjaro juzi.
RAIA wa Marekani Richard Miller na Kara Lee wamefunga ndoa ya kihistoria katika Mlima Kilimanjaro juzi na kuacha watu midomo wazi.

Kara Lee akimvisha pete mumewe Richard Miller.
Wanandoa hao waliwasili nchini wiki iliyopita na kuanza safari yao ya siku saba kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia njia ya Machame Septemba 20, 2014 na…

 Kara Lee akimlisha keki mumewe Richard Miller mara baada ya kufunga ndoa katika Mlima Kilimanjaro juzi.
RAIA wa Marekani Richard Miller na Kara Lee wamefunga ndoa ya kihistoria katika Mlima Kilimanjaro juzi na kuacha watu midomo wazi.

Kara Lee akimvisha pete mumewe Richard Miller.
Wanandoa hao waliwasili nchini wiki iliyopita na kuanza safari yao ya siku saba kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia njia ya Machame Septemba 20, 2014 na kutumia usiku huo katika banda la Machame.
Kara Lee anasimulia hivi: “Katika Sikukuu ya Krismas huko Minnesota nchini Marekani tulivishana pete mimi na mchumba wangu Richard Miller na kuwekeana ahadi kuwa ndoa yetu lazima ifungwe juu ya paa
la Afrika na hiyo sehemu si nyingine zaidi ya Mlima Kilimanjaro”.

Wanandoa hao wakisaini kitabu cha maharusi.
Baada ya hapo, wawili hao walianza mipango ya kutimiza ndoto yao hiyo ya pekee na ya kihistoria kwa kukusanya fedha kwa ajili ya safari yao kuja Tanzania. Wapenzi hao waliwajulisha ndugu na jamaa juu ya uamuzi wao huo ambapo walipata baraka zote za kutimiza ahadi hiyo.
Safari yao ya kupanda mlima huo ilikuwa ikiongozwa na Kampuni ya Utalii ya Zara iliyopo mjini Moshi, Kilimanjaro ambapo Septemba 21 mwaka huu majira ya saa 6 mchana wawili hao waliwasili katika pango
la Shira wakitokea banda la Machame wakiwa pamoja na wenyeji wao tayari kwa ndoa yao hiyo iliyokuwa gumzo kwa watu waliohudhuria.

Mchungaji Aloyce Mbugi kutoka Kanisa la TAG la Victory Christian Centre lenye makazi yake jijini Arusha akiwafungisha ndoa Kara na Richard.
Siku hiyo ya Jumapili, Septemba 21, 2014 Mchungaji Aloyce Mbugi kutoka Kanisa la TAG la Victory Christian Centre lenye makazi yake jijini Arusha alianza ibada ya kuwafanya kitu kimoja Richard Miller na Kara Lee kama mume na mke.
Maharusi hao wakisimamiwa na Ansigar Mtandika na Neema Njau, walianza kula viapo vya ndoa pamoja na kuvishana pete mbele ya mchungaji huyo huku wakiahidi kuwa pamoja katika shida na raha mpaka
Mwenyezi Mungu atakapowachukua.

Wanandoa hao katika pozi baada ya kufunga ndoa.
Baada ya zoezi hilo, wanandoa hao walikunywa shampeni pamoja na waalikwa waliohudhuria tukio hilo la kihistoria na kuhitimisha ndoa hiyo iliyofungwa kwa saa tatu.
Richard na Kara walianza maisha ya mke na mume katika hema na leo wameendelea na safari yao ya kuupanda mpaka kileleni Mlima Kilimanjaro ambapo wamefika kituo cha Baranco. Wanandoa hao
wanataraji kufika kilele cha mlima huo kesho Jumatano na wataanza kushuka kuelekea geti la Mweka Keshokutwa Alhamisi ya Septemba 25, 2014.
“Wana nguvu na wamepania kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro na naamini watatimiza ndoto yao nyingine hiyo," alisema Teophil Karia, mwongoza wageni kutoka Zara Tours.

0 comments: