Usikubali Kuogopa Kumuonyesha Mke au Girlfriend Wako Unampenda Kisa Unaogopa Washkaji Watakuona Bwege
Usikubali kuogopa kumuonyesha mke wako au girlfriend wako unampenda
kisa unaogopa washkaji au ndugu watakusema umekaliwa naye. Ni tabia
mbaya sana unakuta mtu mzima eti anajitamba mbele za wanaume eti “mimi
bwana mwanamke hawezi niuliza niko wapi” sasa ndugu yangu wewe ndio
ulimtongoza mwenyewe tena ulimsumbua hasa msichana wa watu leo hii
anakupigia simu anakuuliza uko wapi unaanza kupanic. Tusifanye vitu ili
kuwaridhisha washkaji huko viringeni…tufanye vitu kuwaridhisha wake
zetu…. imefikia wakati mwanaume usipokaa bar mpaka saa nane au saa saba
usiku unaonekana bwege na ukiangalia ligi ya ulaya sebleni kwako na mke
wako unaonekana bwege pia…au usipokua na demu wa nje eti wewe sio
mjanja. huu ni upuuzu tubadilikeni jamani. ndio sikatai usikae na
washkaji lakini usipitilize sasa. Naona huruma sana unakuta mtu kavaa
lipete likuuubwa la ndoa amekaa bar kwenye kiti anasinzia..jamani ?
0 comments: