1. Lady Jaydee
Uyu dada ndio msanii mwenye washabiki kuliko wasanii wote Bongo, ni
mwanamuziki anayeheshimika na wasanii wenzake karibu wote na wadau
mbalimbali wa muziki na sekta zingine.
Aliyejaribu kumgusa Msanii yoyote anayejaribu kumgusa uyu dada
unapotea yeye, wasanii waliioonja joto ya Jide ni awa wafuatao na
wakapotea
Chidi benzi;
uyu baada ya kuvuma sana akawa anamchokoza uyu dada
kwa kufanya mambo ya kumkosea heshima Komando leo amebakia hadithi,
ameishia kuwa mteja.
Mwana FA;
uyu alikuwa rafiki mkubwa wa Jide na alimshirikisha Jide
kwenye album zake zote, ata maisha ya kawaida walikuwa wakishirikiana
kwenye vingi.
Mwishoni alikuja kumsaliti Jide kwa kutumika na Joseph
Kusaga na Clouds kujaribu kudhoofisha mahudhrio ya show ya Jide ya
kutimiza miaka 10, hii ilizua ugomvi mkubwa kati yao na baada ya hapo FA
akapoteza mashabiki wake wengi sana waliomchukulia kama msanii mwenye
upeo mkubwa.
Ana wimbo mpya mkali sana ‘mfalme’ ila umepotea kwa kuwa FA ameshatoka mioyoni mwa watu.
Mrisho Mpoto
Msanii uyu wa ushahiri alijiharibia baada ya kumtaka Jide amkabidhi
kijiti Lina au Recho wakati wake umepita, na aliyazungumza haya kwenye
jukwaa la fursa.
Baada ya hapo waliomchukulia kama mwanaharakati
ambao ndio walikuwa washabiki wake wakubwa wakambeza na kumpotezea moja
kwa moja.
Mpoto amebaki kupata matangazo ya serikali ila muziki
umeisha na ataki kukabidhi kijiti kwa Mpoki wanaefanya style moja kama
alivyomtaka Anaconda.
Ben Pol
Uyu alimwita Jide mgonjwa wa akili kupitia social
networks, baada ya Jide kumtuhumu kuvunja mkataba wa kutumbuiza show
yake ya kutimiza miaka 10. Kwa sasa Ben ni hadithi iliyopita.
Wapo wengi wengine ni ishu za chini ya kapeti
MR II Sugu aka Nyerere wa Rap
Uyu ndio baba wa Bongofleva na hiphop kwa ujumla. Ni msanii
anayeheshimika kwa misimamo yake ‘tata’ na uwezo wa kupambania mambo
mbalimbali. Historia na mchango wake kwenye muziki wa Tanzania hakuna
anayeweza kumnyang’anya japo kuna waliojaribu ila wakashindwa.
Kwa sasa ameeegemea zaidi kwenye siasa, akiwa kama mwakilishi wa watu wa Mbeya mjini.
Waliomgusa
Mwana FA
Uyu FA alikuwa rafiki mkubwa wa Sugu, aligeuka adui baada ya FA
kujigeuza ngao kwenye ugomvi wa Sugu na Clouds media akisimama kati
kumzuia Sugu asifikishe makombora yake kwa upande wa pili (refer
AntiVirus Saga). Tangia hapo FA alijipoteza ushawishi na zaidi baada ya
kuharibu na kwa Jide, akajibrand upya kama kibaraka.
Roma Mkatoriki
Uyu alimdiss Sugu kwenye wimbo wake wa KKK na ukawa ndio mwisho wa
Roma. Kwa sasa anatoa ngoma zinabaki kuwa habari tu kuwa Roma ametoa
mpya ila zinabuma.
Bwana Misosi
Alimdiss Sugu kwenye kwenye ‘nitoke vipi’ na akafanikiwa kuvuma kwa
muda . Ingawa alikuja kusahihishakauli lakini alipotea yeye akamwacha
Sugu aliyemkashifu .
Joh Makini
Kwenye wimbo wake ‘ manuva’ alimdiss Sugu akisema anafanya harakati
magirini. Kwa sasa Joh anasafiria nyota ya weusi maana nyimbo anazotoa
baada ya hapo zinabuma.
Kuna wengine wengi tu kina Afande sele, Mox, Jafarai na wengineo wote waliomjaribu Sugu wamepotea.
Kifupi hakuna aliyewahi kuwagusa awa manguli akabaki salama.
Swali ni je, Kwa nini imekuwa hivi?

No comments:
Post a Comment