KUMEKUCHA LIGI YA UINGEREZA MAKOCHA WAANZA KUKALIA VITI VYA MOTO

Mshambuliaji
Graziano Pelle aliifungia mara mbili Southampton na kuibamiza vibaya
kikosi kilichocheza vibaya cha Newcastle katika Dimba la Mtakatifu
Mary’s .
Mtaliano huyo alifunga goli lake la kwanza katika dakika ya sita ya
mchezo alipoungansha kwa Kichwa Krosi ilitokea upande wa Kushoto
ikipigwa na Ryan Bertrand’s .
Alifunga bao lake la Nne katika msimu huu baada ya maamuzi mabaya ya Mike Williamson katika safu ya Ulinzi ya Newcastle .
Jack Cork alifanya kazi ya ziada baada ya uzembe uliofanywa na Williamson kabla ya Morgan Schneiderlin Kufunga Bao la nne

Diego Costa amefunga magoli matatu katika mechi yake ya Kwanza
wakitokea nyuma na kuibamiza Swansea na kuendeleza takwimu yao ya
asilimia mia ya ushindi 100% tangu msimu wa ligi kuu uanze .
Swansea ndio waliokuwa wakwanza kupata goli baada ya John Terry
kujifunga akiokoa mpira wa Krosi lakini Costa alisawazisha kabla ya Nusu
ya kwanza ya mchezo kumalizika .
Chelsea’s iliendelea kuwa bora na Costa alifunga akipokea pasi kutoka kwa Cesc Fabregas .
Mshambuliaji huyo wa Uhispania alimtengea mpira Ramires ambaye
alipiga shuti lilompita Lukasz Fabianski na Loic Remy akafunga goli
lake la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo lakini Jonjo Shelvey’s
alifunga goli la kufutia machozi .
Matokeo mengine katika ligi ya uingereza ni kama unavyoyaona hapo chini
0 comments: