KHADIJA KOPA MARAFIKI ZAKE WALIKUWA WAVULANA SHULENI
Khadija Kopa ameanza kuyasimulia maisha yake, amekwenda kuanza shule
huku moyo wake ukiwa na hofu kwa kuona kwamba sasa ni wakati wa kuchapwa
fimbo kama walivyokuwa wengine.
Malkia wa mipasho tanzania, Khadija Kopa
Anaishi na bibi yake, bi Biubwa lakini mara kwa mara mama yake amekuwa akifika hapo kwa ajili ya kumsalimia.Maisha ya bibi yake yakaanza kumfanya kudeka sana kwani hakuwa akichapwa wala kufokewa…
Khadija
Kopa ameanza kuyasimulia maisha yake, amekwenda kuanza shule huku moyo
wake ukiwa na hofu kwa kuona kwamba sasa ni wakati wa kuchapwa fimbo
kama walivyokuwa wengine.
Malkia wa mipasho tanzania, Khadija Kopa
Anaishi na bibi yake, bi Biubwa lakini mara kwa mara mama yake amekuwa akifika hapo kwa ajili ya kumsalimia.Maisha ya bibi yake yakaanza kumfanya kudeka sana kwani hakuwa akichapwa wala kufokewa kitu kilichoonekana kuleta usumbufu hapo baadaye.
ENDELEA....
Siku hiyo nikaoneshwa darasa ambalo nilitakiwa kuwepo na kuanza masomo rasmi. Hakukuwa na mwanafunzi aliyekuwa akisoma, kwa sababu tulikuwa wadogo, muda mwingi tulikuwa tukipiga stori tu na vurugu za hapa na pale.
Katika kusoma kwangu shuleni hapo, nikabahatika kupata marafiki wengi, ila asilimia kubwa walikuwa wanaume. Ninaowakumbuka, mmoja alikuwa Salum na mwingine aliitwa Mohammed.
Hao ndiyo nilikuwa karibu nao, nilicheza nao na kula wote shuleni. Nilipokuwa sina hela, walichokuwa wakinunua tulikula wote kitu kilichonifanya kuwa karibu nao kwa kiasi kikubwa.
Alikuwa akiwaachia madaftari marafiki zake
Kwa sababu nilipenda sana michezo shuleni, kuna siku nyingine tulipotakiwa kurudi nyumbani, niliwakabidhi madaftari yangu wenzangu wanipelekee nyumbani na mimi kubaki shuleni nikicheza.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu, japokuwa nilitakiwa kusoma lakini wakati mwingine michezo ilionekana kuwa bora zaidi ya masomo. Kila nilipokuwa nikirudi nyumbani, bibi alikuwa akiniambia kwa upole kwamba sikutakiwa kuwakabidhi watu madaftari yangu bali nilitakiwa kurudi nayo nyumbani mwenyewe.
BIBI AMDEKEZA
Bibi alinidekeza kama yai, hata pale nilipokuwa nikifanya makosa ambayo nilitakiwa kufokewa au kuchapwa, alikuwa akiniambia kwa sauti ya upole mno. Maisha niliyokuwa nikiishi naye, alionekana kwamba alitaka kunifundisha mengi kuhusu maisha.
Nilifurahi japokuwa na mimi nikaongeza ujeuri zaidi. Hata yale mambo mabaya, kwangu niliyaona mazuri na kuyafanya, bibi akabaki akiniambia maneno ya upole tu, alikuwa akinipenda mno na hakutaka kunikasirisha Khadija mimi.
***
Japokuwa nilikuwa mtoto mdogo lakini niliutambua upendo ambao mama yangu alikuwa akinionesha. Alikuwa mama wa kipekee sana ambaye kila siku ilikuwa ni lazima afike nyumbani hapo na kunijulia hali.
Nilikuwa nikiishi na bibi lakini kama inavyojulikana kwamba damu nzito kuliko maji, nilipokuwa na mama nilijisikia furaha zaidi.
Sikuwa nimemuuliza kuhusu baba yangu kwani mara nyingi alipokuwa akifika hapo nilikuwa nikisahau na hata kama ilitokea kukumbuka, basi ilikuwa ngumu kumuuliza kwani nilikuwa mdogo.
ALETEWA NGUO NA MAMA YAKE
Kudhihirisha mapenzi makubwa aliyokuwa nayo juu yangu, mama alikuwa akiniletea nguo mara kwa mara hata wakati mwingine kuniletea tende.
Naweza kusema kwamba nilikuwa tofauti na wanafunzi wengine. Kidogo, kichwa changu kilikuwa na akili japo hazikuwa nyingi kama za wanafunzi wengine ambao walikuwa wakiongoza darasani.
ALALAMIKIWA KUWA NA MARAFIKI WA KIUME
Mwaka 1977, nilikuwa darasa la tano. Kama kawaida yangu marafiki zangu wengi walikuwa wavulana. Kulikuwa na kundi kubwa la wasichana waliokuwa wakinichukia lakini sikutaka kujali, bado urafiki na wavulana ulizidi kuongezeka huku kila siku nikiendelea kuwa na marafiki wapya.
“Unavaa ushungi halafu unakuwa na marafiki wanaume?” aliniuliza mwanafunzi mmoja wa kike, siku hiyo niliitwa katika kundi la wasichana wenzangu kama kusutwa.“Kwani dhambi?” niliuliza kwa kifupi swali lililowakasarisha zaidi.
Hawakunijibu swali langu, walibaki wakinisonya lakini sikujali.
Naweza kusema nilipenda urafiki na wavulana kwa sababu wengi walikuwa wakijiamini sana tofauti na wasichana kipindi kile.
Nilipokuwa na tatizo, wavulana walikuwa wepesi kunisaidia tofauti na wasichana. Tulikuwa na umri mdogo lakini tayari marafiki zangu wachache wasichana walikwishanionesha kwamba sikutakiwa kuwaamini.
Kila wakati walipokuwa wakikaa, maongezi yao hayakuwa mazuri kitu kilichonifanya niachane nao na kuendeleza urafiki wangu na wavulana.AENDA MADRASA
Nilipokuwa nikirudi nyumbani, nikawa najiunga na Madrasa. Japokuwa nilikuwa nikisoma shule lakini bibi alimshauri mama kwamba sikutakiwa kupata elimu ya dunia tu bali na kuifahamu zaidi dini yangu ya Kiislam.
Kila nilipokuwa nikirudi nyumbani, nilivaa kanga zangu na kujivika ushungi, baada ya hapo, nachukua juzuu na kuelekea Madrasa.Ustaadhi aliyekuwa akitufundisha siwezi kumkumbuka jina lake, ila alikuwa mmoja wa walimu bora kabisa ambaye kila siku alikuwa akihakikisha kwamba tunaelewa na kufanya kile tulichokuwa tukitakiwa kukifanya.
Watoto wengi wa Zanzibar walikuwa wakikusanyika katika Madrasa hiyo na kupata elimu ya Kimungu. Japokuwa nilikuwa nikipenda sana kwenda kusoma chuoni lakini kitu ambacho kilikuwa kikinitesa zaidi kilikuwa ni fimbo tu.
Mwalimu alikuwa akituchapa sana pale tulipoonekana kuleta uzembe katika masomo. Tulichukia lakini mwisho wa siku tukaona kwamba ilikuwa sahihi kwani uzembe wetu ndiyo uliosababisha kuchapwa fimbo hizo.
WENZAKE WAPELEKWA MADRASA KWA NGUVU, AOGOPA
Kulikuwa na matukio mengi yaliyokuwa yakitokea, kulikuwa na watoto ambao kamwe hawakupenda chuo, cha kusikitisha, wengi walikuwa watoto wa mahustaadhi na mashehe wakubwa.
Hao, walikuwa wakifuatwa mitaani na kubebwa juujuu na kuletwa chuoni ambapo walikutana na fimbo nyingi zilizonifanya kuogopa zaidi hivyo kunifanya kuhudhuria chuoni kila siku bila shuruti.
Mpaka kufikia kipindi hicho, sikujua kama nilikuwa na kipaji cha kuimba, nilijichukulia kawaida sana lakini nilipofika darasa la saba, hapo ndipo nilipogundua kwamba mbali na ukimya wangu,
uoga wangu, pia Mungu alikuwa amenipa kipaji cha kuimba ambacho niliamini kingeweza kunisaidia maishani japokuwa sikuwa na uhakika kwa kuwa mambo ya kuimbaimba yalikuwa Bara na si Zanzibar kama ilivyokuwa sasa.
0 comments: