Mchezaji wa Zamani wa man city na sasa Bayern Munich’s Jerome
Boateng amefunga goli la ustadi wa Hali ya juu katika Dakika ya mwisho
wa Mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya timu yake ya zamani
ya Manchester City na kuinyima walau alama moja .
Mlinzi huyo wa zamani wa city Boateng alipiga kiki kali iliyoparazwa
na kumshinda Joe Hart baada ya city kushindwa kuokoa mpira wa kona .
Hart aliokoa michomo kadhaa kutoka kwa kina Thomas Muller, Mario Gotze na Boateng.
City’s walipata nafasi ya Dhahbu katika Dakika za mwisho wa mchezo
pale Sergio Aguero alipomshinda Dante lakini alipiga mpira uliotoka nje
kidogo ya goli .
Kwa
upande wa Chelsea Cesc Fabregas amefunga goli lake la kwanza katika
mashindano ya klabu bingwa barani ulaya lakini halikuweza kumsaidia
kocha Jose Mourinho’s kupata ushindi baada ya Schalke kusawazisha
goli hilo .
Kiungo huyo wa Uispania , 27, aliyejiunga akitokea Barcelona majira
ya kiangazi alifunga goli hilo akipokea mpira kutoka kwa Eden Hazard’s
.
Didier Drogba alipiga shuti ambalo lilitoka nje ya goli na baadae
Klaas-Jan Huntelaar aliipatia goli la kusawazisha timu yake .
0 comments: