Amber Rose aliwashtua mashabiki wake
na Wiz Khalifa baada ya kuripotiwa kutengana na mumewe huyo huku
akifanya taratibu za kupata talaka yake kisheria.
Baada
ya taarifa hizo kusambaa kwenye vyombo vya habari siku mbili
zilizopita, iliripotiwa kuwa chanzo cha yote ni Amber Rose kuchepuka na
mme wa Mariah Carey, Nick Cannon ambaye pia ndoa yake iko katika
sintofahamu.
Hata
hivyo, Amber Rose amethibitisha kuwa Wiz Khalifa alikuwa akimsaliti na
wanawake wengine huku akikanusha vikali tuhuma za kuchepuka na mwanaume
yeyote kwa kipindi chote cha ndoa yao.
Ameendelea kusisitiza kuwa hivi sasa anakijikita katika malezi ya mtoto wao wa kiume, Sebastian.
Amber ameandika tweet kadhaa kupitia twitter kuhusu sakata hilo.
“Please
stop with the fake tales. I would never ever ever cheat on my husband
in a million years I think u guys know this….. Unfortunately my now ex
husband can’t say the same…. I’m devastated and crushed but my main
focus is Sebastian. Thank u for all the support in this hard time.”
No comments:
Post a Comment